.

.

Friday, 9 December 2016

kutoka TFF SUALA LA MCHEZAJI HASSAN RAMADHANI KESSY Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka: 1. Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016. 2. Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba. 3. TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo. 4. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans. 5. Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Haasan Kessy na Klabu ya Simba. 6. Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima. HATUA: Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69[5] ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania.  *Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).* Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dcidi yake.

Friday, 2 December 2016

MAMBO yanazidi kuwa magumu kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu baada ya asilimia ya marejesho ya mkopo huo kwa kila mwezi kuongezeka kutoka 8% hadi 15%. Mabadiliko haya yamekuja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuwa tayari amekwishasaini mabadiliko ya sheria yanayomtaka mwajiri kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu kwa ajili ya kulipa deni lake analodaiwa na Bodi ya Mikopo.  Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Abdul Razaq, wakati akitangaza kutoa siku 3 kwa wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji wa Mikopo, Abdul Ally. Hatua hii imekuja ikiwa wadaiwa hao tayari wamepewa siku 30 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Abdul Razaq, aliyesema wadaiwa hao sugu watachukuliwa hatua kali iwapo hawatarejesha mikopo hiyo ndani ya mwezi mmoja. Katika maelezo yaliyotolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachoendeshwa kupitia mtandao wa facebook wa East Africa Television, Naibu Waziri Manyanya alisema sheria hiyo tayari imesainiwa na siku za hivi karibuni itaanza kutumika. “Hii asilimia 15, kimsingi ninavyofahamu ilishasainiwa, baada ya hapo kuna kuiangalia iendane na kanuni zetu, baada ya kuicheki imeendana na kanuni zetu kama kuna sehemu itahitaji kuboreshwa kidogo haitazidi miezi miwili au mitatu, baada ya hapo tutaweza kutumia hiyo 15%, na asilimia 15 ya safari hii ni tofauti na siku za nyuma, siku za nyuma tulikuwa tunachaji asilimia 8”, alisema Manyanya. Hapo awali wadaiwa hao wa mikopo walikuwa wanakatwa asilimia 8, lakini sheria ya sasa itaruhusu wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kukatwa asilimia 15 ya kipato chao. Pia Manyanya amesisitiza kuwa kwa wale ambao hawajaajiriwa, lakini wanafanya biashara zao wanatakiwa kuwasilisha angalau shilingi 120,000 kila mwezi na kuwashauri kuwa ni vema wakapeleka zaidi ili wamalize haraka madeni yao. Kuhusu wasio na kazi, amesema haiwezekani mtu asome halafu akose shughuli ya kufanya na kuwataka kutafuta shughuli yoyote ya kufanya ili waanze mapema kulipa madeni yao ndani ya miaka miwili baada ya kuhitimu masomo.