.

.

Wednesday, 25 January 2017

*MANARA BLAA BLAA SITAKI KUSIKIA* Kupitia Magic FM *Manara* aongea dhahabu.... 1. Kuna taarifa zimesambaa mie naziita *black propaganda* ujue Hawa jamaa sijui wana nini wanapenda sana kuzusha vitu Mara ndanda wakate rufaa Mara wachezaj simba hawana vibali na Leo wanasema ya polisi dar. 2. Ni kawaida Yangu kutojibu blaablaa za mtandaoni. Ujue Yanga Hawa wanaangaika sana kazi yao *kuangaika angaika tu hawatulii sijajua nini kinawasumbua* watuache tu. 3. Umesikia sasa kabla ya hyo unayosema haijatokea asubuh walianza kusema " Ooonh simba wachezaji hawajapewa mishahara miezi miwili, sasa baada ya Mkude kuja kukanusha hizo taarifa basi wakaja na hilo la Lufunga. 4. Nawaambia hivi Yanga wasijfche nyuma waende tu TFF wakate wao Rufaa maana wanaumia kweli wajifanye tu Polisi Dar. 5. Niwaambie tu wanasimba wasiwe na wasiwasi simba inaenda hatua inayofuata na tupo fiti kuwavaa Azam fc. 6. Nakuuliza wew uwanja wa Jamhuri na uwanja wa Songea Majimaji una tofauti gani? Nijibu sasa mbona unatetemeka. 7. Kesho tunaandika barua na kuipeleka bodi ya Ligi kukataa kucheza kwenye uwanja wa songea kwa maana kuwa uwanja wa Jamhuri na uwanja wa Songea hakuna tofauti yeyote kama wamefunga kule wafunge na Songea. 8. Tusifanyane wajinga kwanini uwanja wa Jamhuri hawakuufunga kabla ya mechi yetu na Mtibwa ila wameona wanaenda kucheza Yanga ndio wanaufungia. Unagundua nini hapo??? 9. Nasisitiza kwamba tunaandika barua na sisi hatuchezi uwanja wa Majimaji hata iweje. 10. Simba tupo vizuri kila idara na tumejipanga kwa hali madhubuti wala hatuyumbishwi na *Black propaganda* Hongera msemaji makini.. Source Magic FM *By Omary Dihile Jr*

Friday, 6 January 2017

Dhhgxnc

Dhhgxnc

Riyad Mahrez mchezaji bora Afrika 6 Januari 2017 Kiungo wa Leicester city Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka. Mahrez mwenye miaka 25 raia wa Algeria aliyeisaidia Leicester kushinda taji la ligi kuu soka England msimu uliopita, tiyari ameshinda tuzo ya mcehzaji bora wa England sambamba na mchezaji bora wa BBC Mshambuliaji wa Senegal na klabu ya Liverpool Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang walikuwa wakiwania tuzo hiyo pia. Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi. Denis Onyango wa uganda na klabu ya Memelodi Sundowns akishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani. Mchezaji bora kwa kina dada imeenda kwa Asisat Oshoala wa Liverpool na timu ya taifa ya Nigeria huku timu bora ya mwaka ikiwa ni Uganda.

Kgdru

Kgdru

Wednesday, 4 January 2017

Simu ambazo hazifanyi kazi tena na WhatsApp 4 Januari 2017 Huduma ya WhatsApp haitumiki tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zinazotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6. Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema inataka kuangazia kustawisha "huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi." WhatsApp, ilipangiwa kuacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu mwishoni mwa Desemba 2016. Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka jana. Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017. Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia. "Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo," kampuni hiyo ilisema. Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa: Android 2.1 na Android 2.2 Windows Phone 7 iPhone 3GS/iOS 6 Simu ambazo wateja wake hawataweza kutumia Whatsapp ifikapo Juni 30, 2017 ni: BlackBerry OS and BlackBerry 10 Nokia S40 Nokia Symbian S60 Wanaotumia simu za aina hiyo wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi. Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia. Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.

Donald Trump asema wafungwa hawafai kuachiliwa Guantanamo Bay 4 Januari 2017 Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema wafungwa zaidi hawafai kuachiliwa kutoka kwa gereza la Marekani la Guantanamo Bay, Cuba. Amesema wafungwa waliosalia gerezani humo ni "watu hatari sana na hawafai kuruhusiwa kurejea kwenye uwanja wa mapigano tena". Rais Barack Obama alikuwa ameapa kuwa angefunga jela hiyo kabla ya kuondoka madarakani na amewahamisha wengi wa wafungwa waliokuwa wakizuiliwa humo. Kwa sasa, wafungwa 60 wamesalia gerezani na ikulu ya White House ilisema baadaye Jumanne kwamba inapanga kuwahamisha wafungwa hao kabla ya tarehe 20 Januari. Bw Trump alikuwa amepinga mpango wa Obama wa kufunga jela hiyo wakati wa kampeni. Mwezi Februari alisema: "Asubuhi hii, nimemtazama Rais Obama akiongea kuhusu Gitmo, sawa, Guantanamo Bay, ambayo kusema kweli, ambayo kusema kweli, hatutaifunga. Wafungwa wawili wa Guantanamo wapelekwa Ghana "Tuaicha iendelee kutumika... na tutawarundika watu wale wabaya huko, niamini mimi, tutawaweka watu wengi huko." Mnamo 17 Desemba, vyombo vya habari Marekani viliripoti kwamba Pentagon inapanga kuwahamisha wafungwa wengine 17 siku chache zijazo. Bw Obama ameidhinisha kuhamishwa kwa wafungwa lakini Bunge la Congress ambalo linadhibitiwa na chama cha Republican limewekwa masharti mengi. Bunge hilo linaitaka wizara ya ulinzi kutoa taarifa kuthibitisha viwango vya kiusalama vimetimishwa angalau siku 30 kabla ya hatua kama hiyo kuchukuliwa. Nchi kadha zimewapokea wafungwa wa zamani wa Guantanamo, zikiwemo Ghana, Senegal, Umoja wa Milki za Kiarabu (UAE), Uganda na Cape Verde. Watu 780 walizuiliwa Guantano tangu 2002, lakini kwa sasa ni 105 pekee waliosalia gerezani. Hamsini kati ya hao wameidhinishwa kuachiliwa huru. Jela hilo ilijengwa na Marekani baada ya mashambulio ya tarehe 11 Septemba mwaka 2001 na hutumiwa na Washington kuwazuilia "wapiganaji maadui". Gereza hilo hugharimu Marekani $445m (£316m) kila mwaka.