.

.

Friday, 14 October 2016

Uchaguzi Marekani 2016 Trump 'alipapasa wanawake kama pweza' 13 Oktoba 2016 Wanawake wawili wameambia gazeti la New York Times kwamba mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump aliwashika kimapenzi bila idhini yao. Mwanamke mmoja amesema mgombea huyo alimshika matiti na kujaribu kuingia mkono wake chini ya sketi yake wakiwa kwenye ndege miongo mitatu iliyopita. Wa pili anasema Bw Trump alimpiga busu bila yeye kutaka katika jumba la Trump Towers mwaka 2005. Maafisa wa kampeni wa Trump wamesema "makala hii yote ni hadithi ya kubuni". Gazeti la New York Times limeanzisha kampeni "ya uongo, na iliyoratibiwa kumharibia jina kabisa", taarifa ya maafisa wa Trump imesema. Jessica Leeds, 74, kutoka Manhattan, ameambia gazeti hilo kwamba alikuwa ameketi karibu na Bw Trump sehemu ya abiria wa hadhi ya juu kwenye ndege wakielekea New York pale alipoinua sehemu ya kupumzishia mkono kitini na akaanza kumshika. Mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 38 wakati huo. "Alikuwa kama pweza .... mikono yake ilinishika kila pahali," anasema. "Ulikuwa ni unyanyasaji." Rachel Crooks alikuwa mpokezi wa wageni katika kampuni ya kuuza ardhi ya nyumba katika jumba la Trump Tower, wakati huo akiwa na miaka 22. Anasema alipigwa busu la lazima na Bw Trump nje ya lifti ya jengo hilo. "Ilikuwa vibaya sana," Bi Crooks ameambia New York Times. "Niliudhika sana kwamba alidhani nilikuwa sina maana kiasi kwamba angefanya hivyo (bila hiari yangu)." Wawili hao hata hivyo hawakuripoti visa hivyo kwa maafisa wa serikali. Hata hivyo, wanasema waliwaambia marafiki na jamaa zao yaliyojiri. Bi Leeds anasema alikasirika sana na alitatizika kimawazo baada ya Bw Trump kumgusa. Anasema mara moja aliondoka eneo la abiria wa hadhi na kwenda kuketi eneo la abiria wa kawaida. Maafisa wa kampeni wa Clinton wamesema simulizi hizo za kuogofya kwenye New York Times zinatilia mkazo "kila kitu ambacho tunajua kuhusu jinsi Donald Trump huwachukulia wanawake". 'Kumshika makalio' Hayo yakijiri, Mindy McGillivray naye ameambia gazeti la Palm Beach Post kwamba akiwa na miaka 23 , Bw Trump alimshika makalio katika kilabu chake cha Mar-a-Lago club jimbo la Florida mwaka 2003. Anasema alikuwa amesimama karibu na mchumba wake wa wakati huo Melania Knauss. Bi McGillivray, ambaye kwa sasa ana miaka 36, anasema hakuripoti kisa hicho kwa polisi. Lakini mwenzake, mpiga picha Ken Davidoff, aliambia gazeti hilo kwamba mwanamke huyo alimwita kando siku hiyo na kumwambia: "Donald amenishika makalio sasa hivi". Maafisa wa Trump wanasema madai ya Bi McGillivray hayana ukweli wowote. Wanawake wote watatu wamesema wanaunga mkono Bi Clinton. Wataalamu waonya Trump atakuwa 'rais mropokaji' Afisa wa UN: Trump ni hatari kwa dunia Ijumaa wiki jana, video iliyopigwa mwaka 2005 ilitokea na kumuonyesha Bw Trump akinena maneno ya kuwadhalilisha wanawake na kuongea kuhusu kuwapapasa wanawake. Aliomba radhi kuhusu matamshi hayo, lakini akasema yalikuwa mazungumzo ya mzaha faraghani. Viongozi wengi wakuu wa Republican, akiwemo Spika Paul Ryan, wameshutumu matamshi hayo. Bw Ryan alisema hatamtetea tena Bw Trump.

Thursday, 13 October 2016

Trump ni hatari kwa dunia, anasema afisa wa Umoja wa Mataifa 12 Oktoba 2016 Maoni ya Donald Trump "yanayokera na kuzusha wasiwasi mkubwa" yanamfanya kuwa tishio kimataifa, Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa mataifa amesema. Zeid Raad al-Hussein ametaja matamshi ya Trump kuhusu kutumia mateso, na msimamo wake dhidi ya 'jamii zilizomo hatarini'. Kampeni ya mgombea huyo wa chama cha Republican imekumbwa na shutuma kali dhidi ya matamshi yake yanayozusha mzozo. Mazungumzo yake ya hivi karibuni kuhusu wanawake yamesababisha mgawanyiko mkubwa kisiasa. Bwana Hussein amesema katika mkutano na waandishi habari Geneva: "iwapo Donald Trump atachaguliwa kwa misingi ya alichokisema tayari - na labda hilo libadilike - nadhani, pasi na shaka anakuwa ni mtu hatari katika matazamo wa kimataifa." Hussein amesema wakati uchaguzi utasabaisha kushuhudiwa ongezeko la visa vya watu kuteswa "au kulengwa kwa jamii zilizopo hatarini katika namna ambayo itasababisha wanyimwe haki zao za binaadamu, basi nadhani ni muhimu kusema hivyo". Kamishna huyo amesema hataki kuingilia uchaguzi huo, lakini ana haki ya kuzungumza. Matamshi ya Trump dhidi ya wahamiaji, hususan raia wanaotoka Mexico, yamezusha hasira kutoka kwa wanaharakati wa kutetea haki za binadamu. Ameahidi kujenga ukuta katika mpaka na Mexico na mwezi Juni 2015 aliwaita wahamiaji kutoka Mexico "wabakaji" na "wauaji". Huenda matamshi ya Hussein yasibadili shutuma kali za tajiri huyo wa New York kuhsu Umoja wa mataifa. "Umoja wa mataifa sio rafiki wa demokrasia," Trump alisema mnamo Machi. "sio rafiki pia kwa hata Marekani, ambako sote tunajua ndio makaazi yake makuu." Ameishutumu hatua ya Marekani kutenga fedha katika kuendeleza Umoaj huo. Mwezi Aprili, alisema: "Ni wapi unapo uona Umoja wamataifa? Je unatatua chochote? Ni kama mchezo wa kisiasa. Umoja wa mataifa- namaanisha fedha tunazotumia katika kuendeleza Umoja wa mataifa."

Tuesday, 11 October 2016

*Kesi bado inaendeleaaaaaa* WANAFUNZI wanne wa ualimu waliomfanyia ukatili wa kumchapa fimbo na kumpiga makofi mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya (Mbeya Day), Sebastian Chinguku (17), wamekamatwa na Jeshi la Polisi. Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Mtinika, walimu hao waliokuwa katika mafunzo ya vitendo katika shule hiyo ambao ni Franky Msigwa, Deo John na Evance Sanga wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) na Sanke Gwamaka wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere walikamatwa wakati tukio hilo lililotokea Septemba 28, mwaka huu katika ofisi ya walimu shuleni hapo likiendelea kuchunguzwa. “Walimu wamekamatwa kwa sababu Serikali ina mkono mrefu na uchunguzi unaendelea kufanyika,” alisema. Mtinika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbeya alisema wamebaini kuwa shule hiyo ina tatizo kubwa la utovu wa nidhamu. Alisema walibaini tatizo hilo baada ya mgomo baina ya walimu na wanafunzi kutokea shuleni hapo jana. Mtinika alisema mgomo huo ulipotokea Serikali iliingilia kati na kufanikiwa kuumaliza baada ya walimu kushindwa kufundisha huku wanafunzi nao wakishindwa kuingia darasani kuendelea na masomo. “Leo (jana) asubuhi tulipata taarifa kwamba baada ya tukio la mwanafunzi Sebastian kutokea walimu wamegoma kuingia darasani huku wanafunzi nao walionekana kutokuwa na mwamko wa kuendelea na masomo hivyo ilitulazimu kufika na kulitatua tatizo hili,” alisema Mtinika na kuongeza: “Ili kuinusuru hali hiyo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbeya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ililazimika kuingilia kati kulimaliza. “Ile shule ni kubwa ina wanafunzi 1,467 na walimu 70 na baada ya kuongea nao tuligundua kuna tatizo la utovu wa nidhamu na Sebastian aliyepigwa naye ni miongoni mwa wanafunzi wasiokuwa na nidhamu na tumewaambia wafuate taratibu za shule.” Alisema kitendo cha tukio hilo kusambaa na kuzua mjadala juzi katika mitandao ya kijamii huku Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, kuingilia kati na kuagiza hatua za kuwafukuza walimu hao na kuwakamata ndicho kilichosababisha walimu na wanafunzi wa shule hiyo kupatwa na mshtuko kushindwa kuingia darasani. “Kwa hiyo tumezungumza na walimu na kuwakumbusha wajibu wao kwa wanafunzi huku wanafunzi nao tumewaambia kutambua wajibu wao pindi wakiwa shuleni likiwamo suala la nidhamu ambalo ndio silaha ya kila kitu,” alisema. Mtinika alisema Serikali inafahamu changamoto wanazokutana nazo walimu lakini ni vema wakafuata taratibu za kisheria kwa sababu tukio hilo lilikuwa wazi na halizuiliki, ushahidi unajionyesha. “Kama mwanafunzi ni mtovu wa nidhamu, taratibu zipo na adhabu za kupewa zimeorodheshwa hivyo hakukua na sababu ya kupigwa kama mwizi jambo ambalo halikubaliki nchini kwa sababu hata Katiba yetu imeelekeza,” alisema. Kuhusu utekelezaji wa agizo la Simbachawene la kuitaka Mamlaka ya Nidhamu ya Walimu kumvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Mbeya Day, Magreth Haule, kutokana na kushindwa kutoa taarifa ya tukio hilo, Mtinika, alisema mwalimu huyo ataendelea na majukumu yake kwa sababu linaendelea kuchunguzwa. Kwa upande wake, Mwalimu Haule, aliyejitetea kuwa hakuwapo shuleni na alimkabidhi majukumu yote Makamu wake, Adonath Nombo, wakati tukio hilo linatokea na alisema kwa sasa hawezi kuzungumza chochote bali anasubiri kutekeleza maagizo yaliyotolewa hadi atakapopewa muongozo mwingine. *WALIMU WAFUNGUKA* Wakizungumzia sababu ya wao kushindwa kuingia darasani, baadhi ya walimu wa shule hiyo walisema mara kadhaa Serikali imekuwa mstari wa mbele kutatua matatizo yanayowapata wanafunzi huku wakiwasahau wao wanaofanyiwa vitendo viovu na wanafunzi. “Hapa sitetei tukio la Sebastian, ila ninapenda kuieleza Serikali hasa viongozi wetu wa juu pale walimu wanapowasilisha matatizo ya wanafunzi au uongozi wa shule unapotoa adhabu kwa wanafunzi kama vile kuwasimamisha shule kwa muda kutokana na matatizo ya nidhamu basi wasiingilie,” alisema mwalimu mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe. *WANAFUNZI NAO WANENA* Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ambao walisema tukio hilo liliwashtua kwa sababu hawakutarajia kama mwenzao angeweza kupatiwa adhabu ya namna hiyo. “Ni kweli mwanafunzi ana makosa hatukatai lakini adhabu ya namna ile hakustahili kupewa kwa sababu sisi tulijua mwalimu amemalizana naye darasani kwa kumchapa viboko vitano kumbe, kipigo kiliendelea” alisema Mwanafunzi. *SEBASTIAN AFUNGUKA* Akizungumzia sakata hilo, Sebastian, alisema adhabu ya pamoja na wanafunzi wenzake aliitumikia kwa kuchapwa viboko vitano lakini alishangaa mwalimu aliyemtaja kwa jina la Franky kumuita pembeni na kuanza kumuuliza maswali ambayo yeye binafsi anadai alimjibu. “Mwalimu Franky aliniita pembeni na kuniuliza kwamba unanikumbuka ? Mimi nikamjibu hapana, akaniuliza mara nyingine, tena kwa msisitizo unikumbuki kweli au ni kiburi? Nikamjibu sikukumbuki,” alisema. Sebastina alisema baada ya hapo mwalimu huyo alimwambia kwamba anakumbuka siku ya mtihani alimwambia avue sweta lake lakini na siku hiyo alimdharau na alimwamuru amfuate ofisini. “Alinipeleka ofisini, huku akiwa na walimu wenzake na kuanza kuniadhibu kwa kipigo ambacho nyinyi wenyewe mmekiona na mbali na hilo walimu hao walinishinikiza niandike barua ikiwa na maelezo kwamba mimi ndiye niliye wapiga walimu jambo nililolifanya kwa kuogopa kufukuzwa shule,” alisema. Sebastian alisema wakati walimu wa kawaida wakilijadili suala hilo alionekana amekosa na kumlazimu kumtamfuta mwalimu ambaye ni jirani yake na kumweleza ukweli wa tukio lote. “Mwalimu huyo alifanya upelelezi wake na kubaini kwamba mimi sikuwapiga walimu bali walimu ndio walinipiga mimi hivyo kuwaita na kunitaka mimi nichague adhabu ya kuwapa lakini niliwaeleza kwamba shule ina utaratibu wake juu ya walimu wa namna hiyo lakini mimi binafsi nimewasamehe,” alisema. *DUCE* Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini mmoja wa wahadhili wa DUCE alisema utekelezwaji wa agizo la Profesa Ndalichako bado haujafanyika na hakuna kikao chochote cha kiofisi kilichofanyika jana kwa sababu kwa sasa chuo hicho kimefungwa. “Mimi sio msemaji lakini naweza kusema haya mambo bado yanaongelewa kwenye korido hapa chuoni kwamba vijana hawa hawana makosa lakini bado hayajajadiliwa kiofisi, kwa bahati mbaya suala hili limetokea chuo kikiwa kimefungwa,” alisema mhadhiri huyo. Alisema mbali na kuwa vijana hao kitaaluma wanaonekana hawajafanya kosa kubwa la kupatiwa adhabu yenye uzito huo lakini agizo la Profesa Ndalichako lazima litekelezwe kwa sababu kwa sasa limekaa kisiasa zaidi. “Kumfukuza mtu chuo sio rahisi kama mnavyofikiria kuna taratibu zake, wale ni wanafunzi wamefanya kosa la kawaida ili wachukuliwe hatua taratibu zilipaswa kuanzia shule husika walipaswa waandike barua ije kwenye uongozi wa chuo,” alisema. Alisema barua hiyo ilipaswa kuwasilishwa katika kikao cha Bodi ya Uongozi wa DUCE na badaye taratibu zingetolewa na adhabu zingefuatwa. Alisema waziri hana mamlaka ya kumfukuza mwanafunzi chuo hivyo uamuzi uliotolewa umekaa kisiasa zaidi na msukumo wa mitandao ya kijamii. *HAKI ELIMU* Shirika lisilokuwa la kiserikali la Haki Elimu limesema tukio la Sebastian ni sehemu tu ya matukio mengi ya ukatili wanayofanyiwa wanafunzi shuleni. Pia lilisema kuwa kuwa matukio hayo ya kikatili yamezifanya shule kutokuwa sehemu rafiki na salama kwa wanafunzi na hivyo kuwa na athari kubwa katika juhudi zao za kujifunza. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage, alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2011 na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kuhusu ukatili dhidi ya watoto unaonyesha kuwa kuna viwango vya kutisha vya kikatili dhidi ya watoto katika shule nyingi nchini. Alisema vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa wanafunzi ni pamoja na vitendo vya kingono na kihisia katika mazingira ya shule za Tanzania na kwamba walimu ndio vinara wa ukatili huo. “Kwa mujibu wa utafiti huo nusu ya wasichana na wavulana ambao wamewahi kunyanyaswa kimwili (kufinywa, kuchapwa viboko na kupigwa mateke) waliwataja walimu kuwa ndio wanyanyasaji wakuu shuleni nchini Tanzania,” alisema Kalage. Alisema wamesikitishwa na kitendo cha ukatili aliofanyiwa Sebastian. BODI YA MIKOPO KUSITISHWA KWA MIKOPO YA WANAFUNZI WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO LA KUMDHURU MWANAFUNZI HUKO MBEYA Katika hatua nyingine, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesitisha mikopo ya elimu ya juu iliyokuwa ikitolewa kwa walimu-wanafunzi hao waliosimamishwa masomo kwa kuhusika katika tukio la Sebastiani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana walimu hao wamepoteza sifa za kuendelea kupokea mikopo. “Mikataba inayosainiwa na wanufaika wa mikopo inawataka wanufaika kuzingatia masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na kuzingatia nidhamu na kufuata sheria na taratibu za vyuo na mamlaka halali,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza: “Kwa mujibu wa taratibu za kukopeshwa, wanafunzi hawa watatakiwa kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mara moja. Bodi ya Mikopo inawakumbusha wanufaika wanaoendelea masomo kuzingatia masharti ya ukopeshwaji na kuheshimu sheria, kanuni taratibu na kuwa mfano mwema katika jamii. “Mikopo na ruzuku zinazotolewa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia wema, waadilifu, na wachapa kazi ili kujenga uchumi imara na ustawi kwa wote.” Habari hii imeandikwa na Upendo Fundisha (Mbeya), Khadia Hamis na Aziza Masoud (Dar es Salaam) Source: Mtanzania

Saturday, 8 October 2016

A[10/7, 00:33] JUVENAL SHIRIMA: Waziri hana mamlaka ya kamfukuza mtu Chuo!Kwa mujibu wa The universities Act No 7 of 2005 hilo ni jukumu la board za vyuo (council) Ndio yenye mamlaka ya nidhamu ya kitaaluma ya mwanafunzi wa Chuo!Hao wafungue tu case kwa sababu watashinda! Pia waziri amehukumu bila kuzingatia utaratibu wa jurisprudence and jurisdictions under the law of natural justice (haki ya mtuhumiwa kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa na mamlaka ya kinidhamu! [10/7, 00:40] JUVENAL SHIRIMA: Kwenye kosa la kupiga na kujeruhi wanapaswa kusomewa shitaka la kula njama kupiga na kujeruhi pamoja na misuse of power!Lakini pia wanaweza kushinda iwapo upande wa jamhuri utashindwa kuwasilisha ushahidi wa kuweza kuprove without reasonable dought kwamba video husikika ni sahihi na ni za tukio husika (based on The law of civil proceedings Act Law of evidence Act and penal code of Tanzania) [10/7, 00:42] JUVENAL SHIRIMA: Ila mimi pia kama Mwalimu siungi mkono kitendo walichokifanya hao walimu wanafunzi [10/7, 00:48] JUVENAL SHIRIMA: Nimekuja kutoa tu mawazo yangu kwa kuwa mama Ndalichako naye katumia mamlaka yake vibaya kuhukumu bila utetezi wala exhibit (without considering The law of natural justice) Kinyume na haki za binadamu kwenye katiba yetu ya 1977 (PRESUMPTION OF INNOCENCE UNDER THE COURT OF LAW) [10/7, 00:52] JUVENAL SHIRIMA: [06/10 21:51] Gibbs: This is off record please. Kiukweli dogo kabla ya pale, alikataa kuchapwa wala kuchuchumaa pamoja na kwamba wenzie wamechapwa ambao wote hawakufanya zoezi darasani alipohojiwa akamjibu vibaya mwal katika kumshika wamchape akampa ngumi ya mdomo mwalimu. Ilibidi Wamchukue wampeleke ofisini lakini mwl aliyepigwa ngumi awali alirudi darasani kutuliza wanafunzi wengine. Alipoona wametulia alianza kurudi ofisini kumbe yule dogo pale ofisini alipoona walimu wamebaki wawili tu akawapa dozi ya ngumi wakamshindwa. Akaanza kutoka nje ya ofisi anakimbia yule mwalimu alikuwa darasani akamuona na kumuwahi ukapigwa mkono kidogo akammudu na kumrudisha ofisini kwa walimu wengine hapo ndio kila mmoja akajikuta anahitaji kumaliza hasira zake. Walimu kadhaa wakiwa wanaugulia maumivu. [06/10 21:51] Gibbs: Unajua kwa huyu dogo yeye aliridhia kichapo alichopewa na walimu ndo maana siku11 toka tukio limetokea wala hajaripoti. Hata home hakwenda kusema kwakuwa anakesi tatu nzito na aliwahi kumjibu hovyo baba yake mbele ya walimu alipokuwa ameenda kutetea asifukuzwe. Achilia mbali hayo ameshavunja tv ya dingi yake home wiki mbili zilizopita. Wiki hili amekamatwa na walimu akivuta bangi shuleni na wenzake. Baba yake anasema simtaki huyu nyumbani kwangu. Hivyo tusiangalie mtu alipojikwaa tuangalie pia source ya kujikwaa. Tunapotoa maamuzi tuangalie mambo kwa ujumla wake....... [10/7, 00:57] JUVENAL SHIRIMA: I think wewe huendagi mahakamani ama pia hufuatilii cases! Kuwepo kwa hizo video mitandaoni hakumaanishi zina qualifications za moja kwa moja za kuwa evidence na exhibit under the court of law! Ili zitumike kama ushahidi na lazima ziwe zinacomply na The law of evidence Act na lazima pia tujiridhishe kwamba Tanzania kama tuna sheria inayoruhusu electronic evidences and exhibits [10/7, 01:04] JUVENAL SHIRIMA: Sujakuambia kwa ubaya wala kukubeza Bali nilitaka ujue tu kwamba sio kila evidence inaweza kufikishwa mahakamani! Ndio maana watuhumiwa huwa wanashinda cases za wazi kabisa! Inategemeana pia na mawakili wa upande wowote [10/7, 01:07] JUVENAL SHIRIMA: Hao wakifikishwa tu mahakamani watakana mashtaka yao! Watapata dhamana then wakiweka wakili ndio mziki unaanzia hapo! Yaani wanaweza pia hata kukana hizo videos! Hiyo ndio law bwana!😋😋

Friday, 7 October 2016

Ukuta umeipotezea Chadema alama nyingi  0               Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akitangaza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam. Picha na Maktaba By Luqman Maloto ,Mwananchi Uamuzi ni kifo au uhai, unaweza kuleta faida au hasara, vilevile kujenga au kubomoa. Kila aina ya matokeo ni zao la uamuzi. Inategemea nini ambacho kiliamuliwa kisha kuleta matokeo husika. Ustawi wa chama cha siasa ni matokeo ya ujenzi wa taasisi, vilevile uamuzi ambao viongozi wake hufanya. Vyama vingi vya siasa havipo hai leo hii kwa sababu ya uamuzi. Uamuzi ili ulete matokeo chanya ni lazima uwe sahihi. Na uamuzi hauitwi sahihi mpaka uamuliwe katika wakati sahihi. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alitangaza vita dhidi ya Uganda katika wakati sahihi ndiyo maana uamuzi ule umebaki kuwa sahihi. Chama cha siasa kwa ukuaji wake lazima kijue mazingira na wakati ili kifanye uamuzi sahihi. Siyo kwamba vyama vya siasa vilivyokufa havikuwa na watu wazuri, hapana, ila vilikosea katika uamuzi. Katika siasa ili chama kiitwe hai lazima kiwe na ufuasi. Wafuasi ndiyo huitwa wanachama na wakereketwa. Kumpata mkereketwa ni sharti hasa umkune kwa sera na matarajio. Ukimwonesha mwananchi matarajio yake, kweli atakipigania chama. Chama cha siasa kinapotaka kipotee haraka hata kama kinakubalika kiasi gani, basi kifanye uamuzi ambao hauendani na wakati. Kifo cha chama cha siasa ni kukimbilia kufanya uamuzi kabla hakijaufanyia tathmini kwa matokeo ya pande mbili, hasi na chanya. Mwongozo wa vyama vya siasa katika kufanya uamuzi wa matukio au ajenda, vinatakiwa kutumia mbinu ya kujichelewesha ili kujiridhisha kuhusu kesho. Ni dhambi kubwa kwa chama cha siasa kufanya uamuzi pasipo kufanya tathmini ya matokeo ya uamuzi wake. Angalizo kwa chama cha siasa ni kama benki; kibiashara inafahamika kuwa benki ikikosea katika uamuzi, inaweza kukera wateja ambao kesho wataamkia kwa watoa huduma na kuhamisha fedha zao. Vivyo hivyo kwa chama cha siasa, kikikosea na kuvunja moyo wanachama, kesho yake utakuta wanachama wanarudisha kadi. Kama ambavyo uamuzi wa benki huchukuliwa kwa kuzitangulia hisia za mteja, inatakiwa pia kwa chama, kumtazama mwanachama kabla ya kufanya uamuzi, maana yeye ndiye mwenye chama. Chadema na Ukuta Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Julai mwaka huu kilitangaza kuunda Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta). Msimamo wao ukawa kwamba Septemba Mosi ingekuwa mwanzo rasmi wa kampeni ya Ukuta. Rais John Magufuli alijibu kuwa hajaribiwi, akasema kuwa wenye kutaka kumjaribu wathubutu. Mwanzoni haikuwa tishio, lakini kadiri Septemba Mosi ilipokuwa inakaribia, ndivyo ambavyo hofu ilitanda. Ukweli upo dhahiri kuwa kundi kubwa la Watanzania, liliamini kuwa Ukuta ungezua machafuko. Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), likatangaza kuwa Septemba Mosi ingekuwa maadhimisho yao ya kutimiza miaka 52 ya kuzaliwa. Kwamba nao wangeiadhimisha siku yao kwa kufanya usafi. Polisi waliahidi kuvunja Ukuta, JWTZ wakasema watazagaa mitaani kufanya usafi, Chadema wakasisitiza kuwa Ukuta ‘ungejengwa’ tu. Watanzania wakajikuta kwenye hofu kubwa. Agosti 31, mwaka huu ilipofika, Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alitangaza kuahirisha Ukuta mpaka Oktoba 31, mwaka huu. Sababu akasema ni kupisha mazungumzo kati ya viongozi wa dini na Rais Magufuli. Waswahili husema “usiku wa deni hauchelewi kukucha”, kutoka Agosti 31 mpaka Septemba 30 ilikuwa kama vile kufumba na kufumbua, mara siku ikawadia. Mbowe akarejea tena kuahirisha Ukuta. Hasara za danadana Hapa nitangulie kusema kuwa tukio au matukio yoyote ambayo yana ishara ya uvunjifu wa amani sikubaliani nayo. Tanzania ni muhimu kuliko wanasiasa na matakwa yao ya aina yoyote. Sioni mahali ambapo Chadema walikusudia kumwaga damu ya Watanzania, ila naona kuwa msimamo wa dola kama ungekutana na shinikizo la chama hicho na Ukuta wao, maana yake hali ingekuwa mbaya. Hivyo niliilaani Septemba Mosi, 2016 kwamba haikupaswa kutokea kutokana na vitisho vya Ukuta na vunja ukuta. Hata ahirisho la Oktoba Mosi, sikukubaliana nalo, maana hali ilishakuwa siyo njema kutokana na mivutano ya kisiasa. Hata ahirisho la mara ya pili alilolitoa Mbowe Septemba 30 pia nililiunga mkono. Pamoja na uungaji mkono wangu, lakini ukweli ni kuwa Chadema imepoteza alama nyingi kupitia Ukuta. Ni vyema kuweka kando furaha yangu na hali halisi. Nimefurahi lakini wanachama na wakereketwa wa Chadema je? Wale walionunua fulana na kutamba kuwa wangeingia barabarani Septemba Mosi na baadaye Oktoba Mosi? Je, ni lini tena Chadema wataaminika watakapoandaa operesheni nyingine? Unapofika hapo ndipo unaona kuwa kama chama wamejitengenezea hali ya kutoaminika. Wakereketwa waliopata moto Septemba Mosi mpaka kuingia gharama ya kununua fulana wameshaakisi hali ya ubabaishaji. Hofu ambayo Watanzania walikuwa nayo kila walipoifikiria Septemba Mosi mwaka huu, ni hasara kwa Chadema kila upande. Watanzania leo wanazungumza kwamba kumbe walikuwa wanaogopa Ukuta bure tu, maana haukuwa Ukuta wa ukweli isipokuwa yalikuwa magirini ya Chadema ili kumtikisatikisa Rais Magufuli. Faida imekuwa zaidi kwa Magufuli kwamba kweli hajaribiwi. Hasara kubwa zaidi ni kuwa chama kinapokuwa na wafuasi waaminifu, hujawa na ari ya kuamini kuwa hakuna linaloshindikana. Baada ya maahirisho mawili ya kalenda kuhusu oparesheni ya Ukuta, watu wameshaona kumbe ulikuwa mchezo wa kutishana na anayetishwa hatishiki kweli. Chukua somo hili la mfano; yupo mtu alikuwa na tabia ya kuwatisha watu kwamba amevamiwa na majambazi wanataka kumuua. Anapiga kelele, majirani wanakusanyika kisha anawaambia kuwa alikuwa anawatania. Alifanya hivyo mara kadhaa mpaka majirani wakazoea, wakajua ni mtu wa utani. Siku moja kweli alivamiwa, alipiga kelele, lakini hakuna jirani ambaye alitokeza. Watu kwenye nyumba zao walinong’ona “huyu naye tumeshamzoea.” Baadaye kikafuata kimya, majirani wakajua alichoka kuita na kuamua kunyamaza. Kulipopambazuka wakagundua kuwa ni kweli jirani yao alivamiwa na kuuawa. Wakaambiana “sisi tulidhani utani kama kawaida yake.” Utafika wakati Chadema wanaweza kuwa na mkazo katika operesheni watakayoandaa lakini watu watapuuza kama majirani ambavyo waliamini jirani yao anawafanyia mzaha. Haipaswi kusahaulika kuwa uahirishaji mara mbili wa Ukuta, umefuata baada ya ahirisho la Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), waliosema wanakwenda kujaa Dodoma ili kulisaidia Jeshi la Polisi, kuuzuia Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM uliomchagua Rais Magufuli kuwa mwenyekiti wa chama hicho. Hiyo ndiyo sababu, hata kabla Sepetemba Mosi haijaahirishwa, wapo watu walitabiri mapema kuwa tukio la Ukuta lingefutwa kama ambavyo lile la kuzuia mkutano wa CCM lilivyofutwa. Wakasema Ukuta ni mkwara kama ambavyo tukio la kuzuia mkutano wa CCM lilivyokuwa mkwara. Ukiyatazama hayo unaweza kuyaona ni mambo madogo yenye kupita, lakini ni mabaya yenye kushusha hadhi na imani kwa watu. Ipo siku Chadema watasema wanaleta tukio lingine lakini watu hawatajali, wataendelea na shughuli zao kwa imani kuwa ni kawaida yao kutishia. Siasa inavyotaka Mwongozo kwa vyama vya kisiasa ni kujiepusha na uamuzi ambao unaweza kukifanya chama kionekane kinadandia hoja au kutangaza agenda na kampeni fulani bila kufanya tathmini ya kina. Chama cha siasa hakitakiwi kubabaisha, maana kina wafuasi. Hupaswa kutangaza yale ambayo yanamaanishwa. Kama ni Ukuta kweli uonekane ukijengwa. Chama chenye tabia ya kutishia kisha kinatokomea ‘kuingia mitini’, hukosa mashiko kwa watu. Siasa hutaka viongozi wa vyama kutumia muda mwingi kutafakari ili kutoa uamuzi ambao hautakuwa wenye kubabaisha. Suala la Ukuta kabla halijatamkwa, lilipaswa kupimwa namna ya kufanikiwa na njia ya kupita. Kuahirishwa mara mbili maana yake Ukuta ulipitishwa bila tathmini nzuri. Kosa la kwanza la Ukuta lilifanyika Julai mwaka huu kwa Kamati Kuu ya Chadema kuketi ndani ya muda mfupi na kuamua. Haukutakiwa kuwa uamuzi wa haraka, ulitakiwa kufanyiwa tathmini ya kina. Kosa la pili lilifanyika Agosti 31 katika kuahirisha. Mbowe hakutakiwa kusema Oktoba Mosi wangeingia mtaani, ni kipindi kifupi mno. Kosa la tatu ni tangazo la Mbowe Septemba 30 kuhusu kuahirisha Ukuta Oktoba Mosi, maana alikosa hoja za msingi za kuushirikisha umma. Mwisho Chadema kipoteza alama nyingi za heshima, maana kimeonekana kinababaisha. Mwandishi wa makala haya ni mwandishi wa habari, mchambuzi wa siasa, jamii na sanaa. Ni mmiliki wa tovuti ya Maandishi Genius inayopatikana kwa anuani ya mtandao www.luqmanmaloto.com

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MUHTASARI WA MKATABA. 1. Bodi ya Wadhamini wa Young Africans Sports Club, (ambayo hapa inajulikana kama Mmiliki”) imeingia tarehe 3 September, 2016 Mkataba wa kukodishwa na kampuni ijulikanayo Yanga Yetu Limited (inayojulikana hapa kama “Mkodishwaji” kwa muhtasari wa maazimio yaliyoafikiwa katika Mkutano Mkuu wa Young Africans Sports Club uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2016 ulitambua kuwa Young Africans Sports Club (anayejulikana hapa kama “YANGA”): 1.1 KWA KUWA, Timu ya Soka ya Mmiliki ni kongwe na yenye mafanikio kuliko timu ya soka nyingine zilizoko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye thamani kubwa kiutamaduni na kwa urithi wa Taifa, licha ya jitihada zake zote, inakabiliwa na changamoto za kifedha katika kuiendesha timu yake ya mpira wa miguu, kwa kuwa na usajili mdogo wa uanachama, ukosefu wa mapato, ya ada za Wanachama, mifumo isiyo na ufanisi ya kiuendeshaji, kushindwa kujipatia kipato cha kibiashara kutoka katika hati miliki na nembo za kibiashara za Timu ya Soka ya YANGA kutoweza kujiendesha kibiashara na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Tanzania (TFF)- ambalo kwa mfululizo linasababisha YANGA kuiendesha Klabu yake kwa hasara na kuwa tegemezi kutoka kwa michango ya wahisani na kwa mikopo na kukabili changamoto hizi; na Mkutano wa Wanachama wa YANGA tarehe 6 Agosti 2016 uliazimia kugeuza hali hii kwa kukodisha Timu ya Soka ya YANGA ambayo ilikuwa inajiendesha kwa hasara na mapato madogo kupitia nembo yake na hakimiliki yake (jina na nembo) kwa muda wa Miaka (10), ili kuikinga Klabu kutoendelea kujiendesha kihasara katika kipindi cha Miaka (10) ya ukodishwaji, ijipange kiuwezo ili Timu ya Soka ya Mmiliki na hakimiliki za jina lake na nembo zitakapo rejeshwa baada ya kukodishwa kwa kipindi cha Miaka (10), YANGA itakuwa inaweza kujiendesha yenyewe na iwe na uwezo wa kifedha na iweze kushindana kikamilifu katika shughuli za mpira wa miguu. 2. Yanga Yetu Limited (inayojulikana hapa kama “Mkodishwaji”) ni Kampuni iliyoundwa ili iweze kuingia katika Mkataba na YANGA ili iweze kutimiza malengo ya Klabu kama yalivyo azimiwa katika Mkutano wa Wanachama wa YANGA uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2016. 3. Baraza la Wadhamini wa Young Africans Sports Club baada ya mazungumzo na Mkodishwaji linapenda kuwafahamisha Wana YANGA kuhusu mambo muhimu yaliyomo kwenye Mkataba Huu ulioingiwa kwa kuzingatia na kwa haki miliki kutolewa kwa Mkodishwaji kwa njia ya Mkataba Huu, kwa kukodisha Timu ya Soka ya Mmiliki na haki zake zote, mamlaka na majukumu yote, jina lake na nembo kwa ajili ya kutumika kiamani na kibiashara katika kuziendesha shughuli za Timu ya Soka ya Mmiliki bila ya kuwa na kuingiliwa katika muda wa Mkataba huu kwa muda wa Miaka (10) kuanzia Tarehe ya Ufanisi ya 1 Septemba, 2016, ila kama utasitishwa kabla kufuatana na matakwa ya Mkataba: 3.1 Mkodishwaji atailipia YANGA deni la Shilingi bilioni kumi na moja na milioni mia sita na sabini na sita tu (Tshs. 11,676 billioni) inayodaiwa kama Mmiliki na Mkopeshaji mmoja. 3.2 Mkodishwaji atailipa YANGA Tshs 100 millioni kwa mwaka ambayo YANGA itawekeza kiwango kisichopungua (90%) ili kuimarisha mtandao wa Matawi yake. 3.3 Mkodishwaji atailipa YANGA katika mwaka wa fedha wowote ule kukiwa kuna faida ya fedha taslim ya asilimia 25% fedha ambayo YANGA itaitumia kujenga uwanja wake wa mpira. 3.4 Mkodishwaji atalipa hasara za uendeshadji zilizoko katika Mkataba kutoka kwenye mfuko wake bila ya kuweka madai kwa YANGA. 3.5 Mkodishwaji ataanza kuwekeza kwa vitega uchumi kuanzia siku (90) ya Mkataba katika mafunzo na vifaa, ambavyo kutakuwepo kiwanja cha mafunzo ya mpira katika sehemu atakayo ona inafaa kwake yeye Mkodishwaji. 3.6 Mkodishwaji atahakikisha kuwa majukumu yote ya kifedha ya Timu ya Soka ya YANGA ikijumlishwa ada ya usajili zinazotakiwa kuanzia Tarehe ya Ufanisi na majukumu mengine ya siku zijazo yanalipwa kulingana na mahitaji ya YANGA mapema kutoka kwenye mfuko wa Mkodishwaji. 3.7 Mkodishwaji atahakikisha kuwa Timu ya Soka ya YANGA haitamaliza chini ya nafasi nusu mwisho wa msimu wa ligi ya Tanzania Premium League wakati ikiwa ndani ya kipindi cha Mkataba. 3.8 Mkodishwaji atahakikisha kuwa Timu ya Soka ya Mmiliki iliyokodishwa katika kipindi cha misimu 3 mfululizo itamaliza ikiwa ni mshindi wa nafasi 2 za juu kwenye Tanzania Premium League. 3.9 Mkodishwaji, kwa kila mwaka atafadhili mashindano ya mpira katika mfumo utakao amuliwa na yeye Mkodishwaji kwa Timu ya Soka kwa vijana wenye umri chini ya miaka (18) na kila Tawi la Wanachama wa YANGA litaalikwa kutuma timu yake kushiriki katika shindano hilo. 3.10 Mkodishwaji atakabidhi kwa YANGA tuzo zozote au Nishani yoyote Timu ya Soka ya Mmiliki ikipata, na kuitaarifu YANGA kabla, pale itakapo wezekana, ili YANGA iweze kumteua mwakilishi wa kupokea tuzo hiyo kwa kuitambua Timu ya Soka ya Mmiliki. 3.11 Mkodishwaji ataingia katika Mikataba yote ya ufadhili au mikataba yaleseni kwa kuitisha zabuni kupitia Zabuni za Umma. 3.12 Mkodiswaji ataunda na kuiendesha Timu ya Mpira wa Miguu ya vijana kulingana na kanuni na miongozo ya TFF. 3.13 YANGA itateua moja kati ya kampuni Tano (5) za Ukaguzi Kongwe Duniani wa Mahesabu zije kukagua kwa kila mwaka hesabu za Mkodishwaji kuhakikisha hakuna ubadhirifu. 3.14 YANGA itakuwa na haki ya kipekee kabla ya Tarehe ya Ufanisi wa Mkataba huu kiwango chochote ambacho kinastahili kupata kutoka TFF, ikiwemo Mkataba wa Azam TV ambao unakadiriwa kuwa shilingi milioni mia tatu (300,000,000) kwa matangazo ya msimu uliopita, mikataba ya ufadhili, madeni ambayo haijalipwa, fedha za zawadi, VAT kutoka TFF na fedha zingine zote zitapewa umuhimu wa nafasi ya kwanza katika matumizi ya kukamilisha majukumu ya zamani ya Timu ya Soka ya YANGA ambayo yalijilimbikiza na hayakuwa wamelipwa. 3.15 Mkataba huu utakapo fikia ukomo, YANGA itakuwa na haki ya kurejesha kile ilichokikodisha. 4. Ilikubaliwa kwamba YANGA: 4.1 Itajitahidi mnamo kipindi cha miaka miwili ya Mkataba itakuwa na Wanachama hai 100,000 na kwa kila Wanachama 100,000 itateua Mjumbe mmoja kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Mkodishwaji. 4.2 Itafanya kila juhudi ya kuongeza ardhi inayohitajika katika Makao Makuu yake yaliyopo mtaa wa Twiga ili iweze kujenga uwanja wa mpira unaofaa, ambao Mkodishwaji atawajibika kuchezea michezo yake ya Timu ya Soka ya YANGA, kwa masharti yatakayo kubaliwa baina ya Pande zote za Wahusika. 4.3 Itakuwa na haki katika wakati wowote ule ndani ya kipindi cha Mkataba kusitisha Mkataba ili mradi imfidie Mkodishwaji hasara zote za nyuma, ilipe malipo yote yaliyofanywa kwa YANGA na Mkodishwaji, inachukua mali zilizowekezwa na Mkodishwaji na kumfidia mapato ya siku zijazo – zote, hizi zikiwa zimetathminiwa na moja ya Kampuni za Wakaguzi (5) Kongwe Duniani. 4.4 Ikiwa Mkodishwaji atakarabati au atatumia mali yoyote ya YANGA ataifidia YANGA kwa masharti yaliyokubaliwa kwa masharti tofauti ya Mkataba Huu. 4.5 Mkodishwaji atakuwa na haki ya kipekee ya kiwakilishi (Exclusive Power of Attorney) kwa YANGA kufanya mikataba na TFF, CAF & FIFA kwa niaba ya YANGA bila ya kuingiliwa kati na YANGA lakini anapaswa atoe taarifa kuhusu uwakilishi huo kwa Baraza la wadhamini, kuanzia Tarehe ya Ufanisi wa Mkataba Huu pamoja na haki ya uwakilishi wa YANGA kwa: i) kuunda Kamati zinazohitajika na TFF, CAF na FIFA kuiendesha Timu ya Soka ya Mmiliki iliyokodishwa ii) kusajili au kulisimamisha benchi la ufundi na wachezaji kutoka Timu ya Soka ya YANGA, iii) Kuwa Msemaji Mkuu wa Timu ya Soka ya YANGA kwa Umma. 5. KUFUNGA. 5.1 Bodi ya Wadhamini wa YANGA inapenda kumshukuru Bw. Yusuf Mehbub Manji kwa kupendekeza masharti bora kuliko yale yaliyoazimiwa na kukubalika kwa Wanachama kwa manufaa ya YANGA, na tunampigia saluti uchangiaji wake usio na choyo kwa manufaa ya YANGA. 5.2 Tungependa kuufahamisha Umma kwamba Bw. Yusuf Mehbub Manji ametaka kujiuzulu kutoka Uenyekiti wa Klabu ili kuepusha mgongano wa kimaslahi, lakini tumelikataa ombi lake hili – kwa vile nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu, Wanachama wameonyesha kwa kura zao kuwa wana imani na uongozi wake, kwa vile wakati wa majadiliano, haweki maslahi yake binafsi juu ya yale ya Klabu, lakini anajaribu kadri iwezekanavyo kuisaidia Klabu kuweza kujitegemea kifedha haraka iwezekanavyo ili kuendelea kushindana katika mpira wa miguu kwa kiwango cha juu zaidi, hapohapo akilinda urithi wa Klabu na utamaduni – sifa ambayo tunaihitaji katika Mwenyekiti wa YANGA na kama akijiuzulu kutoka kwenye Klabu, tutakuwa tumempoteza kiongozi mwenye uzoefu na maadili ya hali ya juu wakati tunapofanya mageuzi ya YANGA. Tunachukua fursa hii kuwafahamisha Wanachama na Mashabiki kuwa kuna kazi nyingi kwa faida ya YANGA ambazo Bw. Yusuf Manji anazifanya ambazo hazionekani mbele ya jamii: kitu ambacho kinahitajika katika Klabu. Tunapenda kuwafahamisha Wanachama na Mashabiki wawe waangalifu na maneno yao, kwa vile kauli za maneno ya matusi zinaumiza na zinawavunja moyo viongozi kama Bw. Yusuf Manji ambao tunafahamu hawagombei nafasi za Uongozi wa ndani ya Klabu, kwa sababu wanachukizwa na kutukanwa na Wanachama na hivyo basi, tunawapa mawaidha Wanachama, kwa manufaa ya Klabu watoe maoni yao kuhusu mambo ya soka na utawala wa soka, na siyo kwa watu na familia zao. 5.3 Sasa tunapenda kuwafahamisha Wanachama wa YANGA na Wapenzi wa YANGA kuwa kilichotiwa saini baina ya Pande Zote ni Mkataba ya kihistoria, na kama yakitekelezwa na pande zote mbili, YANGA itanufaika kwa hali ya juu mno kutokana na mazingatio na ushahidi iliyoupata kupitia Baraza lake la Wadhamini kwenye Mkataba wa ukodishwaji. 5.4 Mwisho, tumeombwa na Bw. Yusuf Manji tutangaze hadharani Mkataba Huu, hata hivyo bado tunajadiliana kama kutangazwa huko kutakuwa kwa manufaa ya Klabu, kwa kuwa, kwa upande mmoja ni vema kuwa na uwazi, lakini kwa upande mwingine washindani wa Klabu yetu wataiga Mkataba wetu kwa manufaa yao. YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO …………………………………………. BODI YA WADHAMINI WA YANGA