.

.

Wednesday, 8 February 2017

SIRI 39 ZA KUWA MILIONEA.

1. Tafuta fursa kila kona.

2. Tumia kipaji chako.

3. Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.

4. Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.

5. Usipoteze muda - jali muda kuliko kitu chochote kwani muda ndio kila kitu, muda ni mali.

6. Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali.

7. Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato.

8. Tafuta maarifa kwa mamilionea mbalimbali duniani - soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa.

9. Jenga urafiki na taasisi za kifedha - mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha - tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri  mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.

10. Kuwa na shauku, kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa.

11. Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo.

12. Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali.

13. Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa - angalia fursa hapo ulipo na wekeza.

14. Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako.

15. Chunguza jamii yako wanakosa bidhaa gani kisha dili na bidhaa hiyo nawe utakuwa milionea.

16. Kuwa na wazo (Business idea): mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha.

17. Fanya vitu wewe mwenyewe - acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu.

18. Kuwa na malengo - kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo.

19. Kuwa na moyo wa ujasiri - usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.

20. Kuwa karibu na matajiri -usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.

21. Mtangulize Mungu -mwabudu, msifu, mtolee sadaka, saidia masikini, wajane, wagonjwa, jenga nyumba za ibada. Mungu ndio kila kitu mtegemee yeye.

22. Fanya vitu kitofauti; fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk. Mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi nk.

23. Acha woga - jaribu biashara yoyote, woga wako ndio umasikini wako, usiogope kukosolewa unapokosolewa ndio unajifunza. Usiogope mikopo, mamilionea wengi hufanya mambo ambayo wewe unayaogopa.

24. Kuwa na mtazamo chanya - usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.

25. Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.

26. Kuwa na mipaka katika mambo yako - usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni bidhaa zao hawapangiwi na mtu.

27. Dili na watu wenye kipato kidogo na kati katika biashara zako; mamilionea wengi hulenga mahitaji ya watu wa hali ya chini ambao ndio wengi hapa duniani. Baadhi ya mahitaji ya watu wa hali ya chini ni;

(a) Vyakula na vinywaji.
(b) Vifaa vya ujenzi.
(c) Vifaa vya umeme.

28.Kuwa mwaminifu -mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.

29. Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako - waulize  watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.

30. Kuwa na plani katika kazi zako kila siku.

31. Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe.

32. Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja.

33. Ubunifu ni muhimu sana - fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini - kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu nk.

35. Nunua hisa katika mabenki, makampuni mbalimbali: Mamilionea wengi hununua hisa hivyo humiliki mabenki na makampuni mbalimbali.

36. Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni. Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli.

37. Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea.

38. Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea - kila binadamu anaweza kuwa milionea.

39. Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa - kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemavu nk.

HITIMISHO;
Shujaa mwenzangu, kuwa milionea inawezekana kama mimi na wewe tukifuata njia hizi 39 zinazotumiwa na mamilionea wengi duniani..

Cheche za Manji πŸ‘‡

Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.

Manji: Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.

Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukuahukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.

Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.

Manji: Na katiba inasema kila mtu ana haki yake, Ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.

Manji: Ukinishutumu mimi ni mpumbavu tu wewe.

Manji: Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari.

Manji: Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.

Manji: Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kufungu 32 pia. Vinanilinda.

Manji: Nataka nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.

Manji: Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.

Manji: Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi kukubali.

Manji: Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.

Manji: Kwanini RC Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie?

Manji: Hiwezi kuniita mimi kama mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.

Manji: Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania.

Manji: Kama unataka msaada omba msaasa sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65 nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Saa tano usiku nitoke? Sina kazi nyingine za kifanya?

Manji: Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilling moja. Unanihusisha mimi jina langu nloachiwa na baba kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka yako?

Manji kapanic....!πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”

AFCON 2019 QUALIFIERS SET

GROUP A
Senegal
Equatorial Guinea
Sudan
Sao Tome/Madagascar

GROUP B
Cameroon
Morocco
Malawi
Comoros/Mauritius

GROUP C
Mali
Gabon
Burundi
Djibouti/South Sudan

GROUP D
Algeria
Togo
Benin
The Gambia

GROUP E
Nigeria
South Africa
Libya
Seychelles

*GROUP F*
Ghana
Ethiopia
*Sierra Leone*
Kenya
*Aaaaaaa Salone we go qualify yaaa*πŸ‘†πŸ‘†

GROUP G
DR Congo
Congo
Zimbabwe
Liberia

GROUP H
Ivory Coast
Guinea
Central African Republic
Rwanda

GROUP I
Burkina Faso
Angola
Botswana
Mauritania

GROUP J
Tunisia
Egypt
Niger
Swaziland

GROUP K
Zambia
Mozambique
Guinea-Bissau
Namibia

GROUP L
Cape Verde
Uganda
Tanzania
Lesotho

NOTE: The 12 group winners will qualify alongside the three best runners-up plus Cameroon who will automatically join the qualified teams as host of the competition and together make up the 16 nations for the tournament.
The polling also suggests that should Cameroon top their group, the second-placed side in Group B will have to contest the finals.
The qualifying matches kick off in June and end in November 2018.

Friday, 3 February 2017

ROHO NYEUPE: Simba ikikosa ubingwa, Aveva na jopo lake wajiuzulu

By GIFT MACHA

Baada ya kuifuatilia timu hiyo kwa muda mrefu sasa nimejiridhisha kuwa kama isipotwaa ubingwa msimu huu rais wa timu hiyo, Evans Aveva na jopo lake la uongozi wanapaswa kubwaga manyanga ili timu hiyo itafute maisha mapya.

KUKUBALI kushindwa sio kosa. Mwanadamu mwenye fikra chanya akiona jambo linamzidi uwezo ama linamtatiza hukubali kuomba msaada kwingine ama kuachana na jambo hilo. Wakati mwingine maisha hayahitaji kulazimisha sana.

Nimekuwa nikifuatilia soka la Tanzania siku hadi siku. Nazifuatilia Simba, Yanga na Azam. Nazifuatilia Majimaji, JKT Ruvu, Stand United na hata Lipuli ambayo inalalamikiwa kuwa inataka kupanda Ligi Kuu kwa njia ya mkato. Kwa kifupi nafuatilia kila eneo.

Hata hivyo, leo sitaki kuzungumzia soka lote, nataka kuijadili Simba. Baada ya kuifuatilia timu hiyo kwa muda mrefu sasa nimejiridhisha kuwa kama isipotwaa ubingwa msimu huu rais wa timu hiyo, Evans Aveva na jopo lake la uongozi wanapaswa kubwaga manyanga ili timu hiyo itafute maisha mapya.

Yawezekana Aveva ni kiongozi bora. Yawezekana jopo lake la uongozi linaundwa na watendaji wenye weledi mkubwa, lakini kama atashindwa kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu ama la FA ni wazi kuwa wote wanapaswa kuachia ngazi. Hicho ndicho kitu pekee wanachotakiwa kukifanya mwishoni mwa msimu na inaweza kuwajengea heshima Msimbazi kuliko kuendelea kubaki.

Ifahamike kuwa tangu Aveva na wasaidizi wake wamechaguliwa kuongoza Simba mwaka 2014, timu hiyo imeshinda taji moja, ni lile la Mapinduzi mwaka 2015. Simba haijawahi kumaliza katika nafasi hata ya pili Ligi Kuu chini ya uongozi wa Aveva. Hakuna mafanikio ya uwanjani ambayo Aveva na jopo lake wanaweza kujivunia mpaka sasa.

Msimu huu ulionekana kama unaweza kuwa wa neema kwa timu hiyo, lakini mambo ni kama yanaanza kuwa magumu. Simba baada ya kucheza mechi 13 bila kupoteza, maisha yake yamebadilika ghafla na sasa haina uhakika tena wa kushinda mechi.

Licha ya Simba kutengeneza wigo wa pointi nane na Yanga iliyokuwa katika nafasi ya pili, timu hiyo tayari imeshushwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu na inashika nafasi ya pili. Hofu ya kubadilika kwa upepo huo ndani ya muda mchache inazua hofu kama ni kweli Simba inaweza tena kupindua meza na kushinda taji hilo.

Yawezekana uongozi ukajivua lawama kwa madai kuwa benchi la ufundi la timu hiyo ndio linapaswa kulaumiwa, lakini hilo haliondoi ukweli kwamba utendaji wao utakuwa umefikisha miaka mitatu bila kuleta mabadiliko yoyote ya maana.

Kama unakuwa rais wa timu kwa miaka mitatu na timu yako haijashinda taji lolote la maana. Timu yako haijapata tiketi yoyote ya uwakilishi wa michuano ya kimataifa, uongozi wako una thamani gani? Unakuwa kiongozi unayewaongoza watu kuelekea wapi? Motoni? Sidhani!

Matatizo yanayoikumba Simba sasa hasa katika safu yao ya ushambuliaji yanatokana na uongozi kushindwa kufanya kazi yao vizuri, hasa kamati ya usajili. Ikumbukwe kuwa Kocha Joseph Omog alipendekeza timu hiyo isajili straika mwenye uwezo wa juu ili kuimarisha safu hiyo ambayo tayari ilikuwa inasuasua chini ya Frederick Blagnon na Laudit Mavugo ambao walifunga mabao matano tu katika duru lote la kwanza.

Uongozi wa Simba baada ya kupitia taarifa ya Omog ulifanya kituko kimoja. Ulikwenda kumsajili straika, Pastory Athanas kutoka Stand United ambaye katika duru lote la kwanza alifunga bao moja tu. Huu ni utani uliopitiliza. Huyu ndiye straika wa maana aliyemtaka Omog? Anafahamu Aveva na jopo lake.

Baada ya hapo Simba ikaenda kumsajili kwa mkopo, Juma Liuzio kutoka Zesco ya Zambia. Bahati nzuri wiki moja kabla ya kusajiliwa kwa Liuzio, Mwandishi wa Mwanaspoti, Olipa Assa alifanya makala na mchezaji huyo ambapo alikiri kuwa ana maisha magumu katika kikosi cha Zesco na amekuwa akichezeshwa kwa dakika kati ya 12-15 tu.  Kwa msimu wote uliopita akiwa Zesco Liuzio alikuwa amefunga mabao matatu tu. Maneno haya aliyasema kwa kinywa chake na wiki moja baadaye alikamilisha usajili wa kujiunga na Simba. Unajiuliza tena, huyu ndiye yule straika wa kiwango cha juu aliyempendekeza Omog? Utani mwingine huo. Uzuri ni kwamba namba huwa hazidanganyi. Athanas hajafunga bao hata la kuotea katika mechi tano za Ligi Kuu alizoichezea timu hiyo. Straika huyo amefunga bao moja tu dhidi ya timu ya daraja la kwanza, Polisi Dar katika mchezo wa FA. Pengine ndio timu anazoweza kuzifunga.

Liuzio naye hajafunga bao hata la kuotea katika mechi nne za Ligi Kuu alizocheza. Alifunga bao moja pekee katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi. Je huyu ndiye ‘masia’ tuliyeambiwa tumsubiri? Anafahamu Aveva na jopo lake. Katika mazingira kama haya ni wazi kuwa safu hiyo ya uongozi wa Aveva kama haitafanya juhudi za kupata tiketi ya mashindano ya kimataifa ama kushinda ubingwa, haipaswi kuendelea kuiongoza Simba. Itakuwa ni muda muafaka kupeana mkono wa kwaheri.

Thursday, 2 February 2017

Kwa mujibu wa Biologia, baada ya tendo la kukutana kimwili takribani mbegu milioni 200 hadi 300 hutolewa na mwanaume...halafu zote huanza kupiga mbizi kuogelea kwenye njia safarini kukutana na yai la kike. Ajabu ya kwanza ni kwamba sio zote 200 - 300  ambazo hufanikiwa kulifikia yai( nyingi huchoka na kufia njiani maana si mashindano ya mchezo mchezo). Ajabu ya pili ni kwamba kati ya hizi 300 zinazofanikiwa kufikia yai, ni moja tu..moja tu itakayoshinda nakufanikiwa kupenya na kurutubisha yai, na kwa mantiki hii ILIYOSHINDA NI WEWE HAPO.
 Umewahi kuwaza kuhusu hili vizuri?
Yaani ulishindana mbio hizo ukiwa huna macho na ulishinda, ulishindana bila elimu na ukashinda,ulishindani bila hata cheti chochote wala msaada wa yeyote ....na UKASHINDA
Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?
Tena sasa uko na macho yote, miguu, sasa Unamjua Mungu, sasa ukiwa na plan,ndoto na maono.
Kumbuka ULISHASHINDA toka tumboni huna sababu ya kuwa na hofu yeyote, PAMBANA