MBUNGE
wa Mpanda Mjini, Said Arfi, jana aliwaaga wapiga kura wake akiwaeleza
kuwa uanachama wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) utakoma
mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge la 10 mjini Dodoma.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Kashato
mjini hapa jana, Arfi, aliyekiwakilisha chama hicho kwa miaka 10
mfululizo, aliwaambia wananchi kuwa jimbo hilo litakuwa wazi wakati
wowote wiki ijayo.
“Kama
Chadema wana ubavu, waje walikomboe jimbo hili. Mimi ninaifahamu
Chadema kuliko mtu yeyote mkoani Katavi kwani nilikuwa Makamu Mwenyekiti
(Bara), na sasa nitamuunga mkono yeyote anayefaa kuwa mrithi wangu,” alisema Arfi na kushangiliwa.
Mkutano
huo uliohudhuriwa na umati mkubwa, ulikuwa chini ya ulinzi mkali wa
polisi kutokana na kuzagaa kwa taarifa za kutaka kufanyiwa fujo kwa
Mbunge huyo na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema.
Arfi alisema hatogombea tena Mpanda Mjini; “Lakini
nipo tayari kuvaa shati la kijani au la zambarau kumpigia debe mgombea
yeyote katika jimbo hili. Ninawajua Chadema na kama wakiendelea
kunifuatafuata, nitasema yote.”
Kauli
hiyo ilitafsiriwa kuwa Arfi sasa atafanya kampeni akiwa CCM au ACT
Wazalendo dhidi ya Chadema katika Jimbo la Mpanda Mjini, ambalo kabla
yake halikuwahi kutawala na Mbunge mmoja kwa miaka 10 mfululizo.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Arfi kuweka hadharani mustakabali wake kisiasa,
lakini kauli yake ya kuwa tayari kuvaa shati la kijana inakwenda tofauti
na fununu zilizozagaa mjini hapa kuwa huenda akajiunga na ACT
Wazalendo, chama kinachoongozwa na swahiba wake, Zitto Kabwe.
Ikumbukwe
kuwa mara baada ya Chadema kutangaza kumvua nyadhifa zote Zitto
takriban miaka miwili iliyopita, mara moja Arfi alitangaza kuajiuzulu
nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema.
0 comments:
Post a Comment