Simba imetoa kipigo cha mbwa mwizi jana baada ya kuichapa timu ya
Majimaji ya Songea ‘wanalizombe’ kwa goli 6-0 kwenye mchezo wa ligi kuu
ya Vodacom Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es
Salaam
Vijana wa Msimbazi walianza kupata goli lao mapema kutoka kwa
mchezaji wao chipukizi Ibrahim Ajib aliyetupia goli tatu pekeyake
(hat-trick).
Kwenye mchezo huo Simkba SC ilianza mchezo kwa kasi kwa kuishambulia
mara kwa mara timu ya Majimaji na kupelekea kupata magoli ya mawili ya
haraka katika dakika 15 za mwanzo, dakika ya nane na dakika ya 14 yote
yakifungwa na Ajib.
Dakika za 15 za katikati ya kipindi cha kwanza mchezo ulitulia na
Majimaji wakaonesha uhai kidogo na kufanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa
lakini safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Stamili Mbonde ilishindwa
kutumia vyema nafasi hizo kuipa goli Majimaji.
Sunday, 1 November 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment