Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kupata
bao mapema kabisa katika kipindi cha kwanza mara baada ya kiungo Mbrazil
Ramires kuunganisha kwa kichwa krosi iliyochongwa na Cesar Azpilicueta
mnamo dakika ya 4 na kuipa Chelsea bao la kuongoza.
Ndoto za Chelsea zilizimwa mnamo dakika
ya 45 na Mbrazil Coutinho baada ya kuuchinja mpira kwa uzuri na kumwacha
kipa wa Chelsea Begovic akiwa hana la kufanya.
Coutinho tena alishindilia msumari wa
pili kwa Chelsea baada ya kupiga shuti kali na kutinga moja kwa moja
wavuni mnao dakika ya 74.
Ndoto za Chelsea zilizimwa kabisa mnamo
dakika ya 83 na Christian Benteke ambaye aliingia kuchukua nafasi ya
James Milner na kuipa Liverpool goli la tatu lililopeleka machungu
makubwa kwa Chelsea huku presha ikizidi kumuendea Mourinho baada ya timu
hiyo kuwa na matokea mabovu tangu mwanzo wa msimu huu, wakiwa nafasi ya
15 mpaka sasa.
Continho akifunga goli la pili
0 comments:
Post a Comment