.

.

Sunday, 6 December 2015

KOCHA wa Simba Dylan Kerr, amesema amefurahishwa na usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Paul Kiongera.
Kiongera ni mmoja wa wachezaji walioongezwa kwenye dirisha dogo la usajili na Simba baada ya timu hiyo kuonesha upungufu katika baadhi ya nafasi kwenye mechi tisa za mzunguko wa kwanza.
Akizungumza na gazeti hili, Kerr alisema anamhitaji mshambuliaji huyo ili aweze kumwelekeza namna na kucheza kwa kushirikiana na Hamisi Kiiza kwenye ushambuliaji. “Nimefurahi sana kwamba tayari amejiunga na sisi na sasa ni jukumu langu kuwaunganisha na wenzake,” alisema Kerr.
Alisema ujio wa mchezaji huyo ni fursa nzuri katika maandalizi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Jumamosi.
Alisema amekuwa akiweka mkazo mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji kwa sababu kwake hiyo ndiyo sehemu muhimu ambayo inaweza kuwapa ubingwa msimu huu kama watafunga idadi kubwa ya mabao.
Alisema kuongezeka kwa Kiongera na Brian Majwega, ana uhakika atakuwa amemaliza tatizo la mabao lililojitokeza katika mechi za awali za ligi hiyo. Kocha huyo alisisitiza kuwa ujio wa wachezaji hao utabadilisha kikosi chake katika ushambuliaji na kuwa na safu inayotisha katika kufunga.
Kiongera alirudishwa KCB na Simba baada ya kupata majeraha makubwa ya goti msimu uliopita na timu hiyo kumpeleka India kwa ajili ya matibabu na baada ya hapo ilimruhusu acheze kwa mkopo kwa makubaliano ya kumrudisha atakapopona.K

0 comments:

Post a Comment