.

.

Friday, 6 May 2016

MSIBA MWINGINE KATIKA SOKA

 taarifa za kusikitisha kwa taifa
la Cameroon , usiku wa May 6 2016 Cameroon
na Afrika kwa ujumla ilipata taarifa za
kushtusha, baada ya kupokea taarifa za kifo
cha kiungo wa kimataifa wa Cameroon
aliyekuwa anaicheze Dinamo Bucuresti Patrick
Ekeng .

Ekeng enzi za uhai wake
Ekeng amefariki baada ya kuanguka uwanja
dakika ya 70 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu
Romania uliokuwa unahusisha klabu yake ya
Dinamo Bucuresti dhidi ya Viitorul, mchezo
ambao ulikuwa unarushwa live kwenye TV,
tukio la Ekeng kuanguka limetokea wakati
akiwa kasimama peke yake bila ya mpira.

Mbia alipost picha waliyopiga pamoja wakiwa
timu ya taifa ya Cameroon
Taarifa za kifo cha Ekeng ambaye
zilithibitishwa masaa mawili baada ya
kufikishwa hospitali, zinakuja baada ya
miaka 13 toka Cameroon impoteze kiungo
wake Marc-Vivien Foe kwa stahili kama hiyo,
tukio ambalo lilitokea June 26 2003 wakati
wa michuano ya Kombe la mabara iliyokuwa
inafanyika Ufaransa na mchezo ulikuwa dhidi
ya Colombia .

Beki wa Arsenal Bellerin na mshambuliaji wa
Man United Anthony Martial ni miongoni mwa
mastaa walioguswa na kifo cha Ekeng

Ekeng alizaliwa March 26 1990 na amefariki
akiwa na umri wa miaka 26 baada ya
kuanguka uwanjani, Ekeng ndio alikuwa
kaanza kupata nafasi katika kikosi cha timu
ya taifa ya Cameroon ya wakubwa, muda
mchache baada ya taarifa za kifo chake
kuthibitika, mastaa wa soka walianza kupost
na kuonesha huzuni kwa taarifa hizo.

0 comments:

Post a Comment