.

.

Friday, 6 May 2016

KWANINI SIMBA NI TIMU BORA ZAIDI TANZANIA KIMATAIFA.?

By Malisa GJ
(Kwa msaada wa Samuel Samuel na gazeti la Mwanaspoti).!

Baada ya takwimu za klabu bora Afrika kutolewa na shirikisho la Soka Afrika (CAF) kumeibuka sintofahamu juu ya takwimu hizo na kufikia hatua ya baadhi ya mashabiki wa vilabu vya soka kuwaita CAF kuwa ni "jipu".

Watu wanahoji iweje Simba iwe ya 39 na Yanga ya 55 wakati Simba ina miaka mitatu haijashiriki ligi yoyote iliyoandaliwa na CAF? Wengine pia wanahoji imekuaje timu ya Al-Ahly ya Misri kuishinda timu ya TP Mazembe ambayo ndio klabu bingwa ya Afrika kwa sasa?

TUANZE NA HILI LA YANGA vs SIMBA.

Simba kwa ujumla wake imeshiriki michuano yote inayoandaliwa na CAF mara 28 sambamba na Yanga ambayo nayo imeshiriki pia mara 28. Rekodi hizi ni sawa na Zamalek wao pia wameshiriki michuano ya CAF mara 28. Timu iliyoshiriki mara nyingi ni Al-Ahly imeshiriki mara 36!.

#KlabuBingwa
Simba SC wameshiriki Champions League mara 16 wakati Yanga wameshiriki mara 20!. Lakini hapa Simba anabeba pointi nyingi mbele ya Yanga kwa sababu katika mara 16 walizoshiriki walifika mbali tofauti na Yanga ambao katika mara zote 20 walizoshiriki waliishia kutolewa raundi za mwanzo.

Hii inadhihirishwa na Performance points ya timu hizi mbili kwenye michuano ya klabu bingwa. Perfomance points ya Yanga kwenye kombe hili ni alama 29 wakati Simba ni 34. Yani Simba iliyoshiriki mara 16 ina points 34 na Yanga iliyoshiriki mara 20 ina points 29.

Simba kkt mara 16 walizoshiriki wamefika robo fainali mara 2 (1972 na 2003), nusu fainali mara moja (1974), raundi ya pili mara 10 na kutolewa raundi ya kwanza mara 3. Yanga haijawahi kufika nusu fainali, robo fainali imefika mara mbili (1969 na 1970), raundi ya pili mara 10 na kutolewa raundi ya kwanza mara 8. Hapa hata umlete "Jerry Muro" lazima akubali kuwa amezidiwa points.

Lakini points nyingine Simba walizipata mwaka 2003 walipofanikiwa kumtoa bingwa mtetezi Zamalek kwenye michuano hiyo. Kwa kawaida anayemtaoa bingwa mtetezi kwenye mashindano hupata "credits" nyingi katika ranking. (hata FIFA hutumia kanuni hii). Na kilichoisaidia Simba ni kwa kuwa waliitoa Zamalek kule kwao Misri sio hapa bongo. Hii inawaongezea credits.

Yanga hawajawahi kumtoa nje ya mashindano bingwa Mtetezi, wacla mshindi wa pili. Kwa kawaida Yanga imekua ikizitoa timu ndogo ambazo haziwapi credit yoyote.

Wakati Yanga imeishia robo fainali kwny michuano ya klabu bingwa Afrika Simba imewahi kufika nusu fainali mwaka 1974 na kutolewa kimizengwe Mehala El Kubra ya Misri.

#KombeLaKagame
Kama haitoshi Simba ndiyo inayoongoza kwa kushinda kombe la Kagame mara nyingi zaidi kuliko Yanga. Hadi sasa Simba imechukua Kombe hilo mara 6, na Yanga mara 5. Hichi ni mojawapo ya kigezo kilichowafanya CAF kuwapa Simba alama za juu kuliko Yanga.

#KombeLaShirikisho
Tuingie kombe la shirikisho. Hapa Simba SC ameshiriki mara 8 wakati Yanga ameshiriki mara 6 hii ni credit kwa Simba. Simba katika kombe hili wana alama 9 kwa perfomance yao wakati Yanga wamepewa alama 1.

Hii inatokana na ukweli kwamba kati ya mara 8 Simba ilizoshiriki imefika mbali tofauti na Yanga iliyoshiriki mara 6 lakini ikaishia kutolewa mapema.

Mwaka 1993 Simba ilifikia Fainali za kombe la hilo ambapo ilicheza na Stela Abidjan ya Ivory Cost. Katika fainali hiyo Simba ilitoka droo ya bila kufungana mjini Abidjan lakini ikakubali kipigo cha 2-0 jinini Dar.

Licha ya Simba kupoteza mchezo huo lakini inashikilia rekodi ya kuwa timu pekee Tanzania kufika fainali za michuano hiyo. Yanga hawajawahi kufika fainali za michuano hiyo, nusu fainali wala robo fainali. Mara zote walizoshiriki wametolewa ktk hatua za makundi. Hiki ndicho kigezo kinachofanya Simba kupewa "points 9" na Yanga kupewa "points 1" kwenye category hii.

#KuuzaWachezajiKimataifa
Simba imeizidi Yanga kwa kuuza wachezaji bora kimataifa. Simba ndiyo iliyomuuza Mbwana Samatta kwenda TP Mazembe na Emanuel Okwi kwenda Etoile Du Sahel ya Tunisia. Yanga haijawahi kuuza mchezaji yoyote mwenye viwango kimataifa. Baadhi ya wachezaji wa Yanga huishia kufanya majaribio Uarabuni na kuridishwa nchini kwa kushindwa kufikia viwango.

Kwa ujumla haya ndiyo yanaifanya Simba kuwa ya 39 ktk timu bora Afrika na Yanga kushika nafasi ya 55.

KUHUSU TP MAZEMBE.!
TP Mazembe kwa ujumla wake imeshiriki mara 26 ktk michuano yote ya CAF huku timu ya Al-Ahly ilishiriki mara 36. Kwa kigezo hiki Mazembe anazidiwa points na Al Ahly.

Katika ligi ya klabu bingwa Afrika, Al-Ahly imeingia fainali mara 10 na kuchukua kombe hilo mara 8, ambapo ni mwaka 1982, 1987, 2001, 2005, 2006, 2008, 2012, na mwaka 2013.

Wakati huohuo TP Mazembe imeingia fainali za klabu bingwa Afrika maraa 7 na kufanikiwa kuchukua kombe mara 5, yani mwaka 1967, 1968, 2009, 2010 na 2015. Hadi hapa haihitaji "degree" kujua kwamba TP Mazembe imeachwa mbali na Al Ahly.

NB:
Acheni ushabiki "mandazi" wa kulumbana pasipo kuwa na facts wala evidence. Pia msidhani kwamba timu ikichukua kombe mwaka huu basi ndio inakuwa no.1 kwenye ranking. Hakuna huo ujinga.

Records za timu zina matter sana ktk ranking. Hii ina maana kwamba Simba au Yanga zikifika fainali za klabu bingwa leo na kuchukua kombe haziwezi kuwa za kwanza kwenye list.

Kuhusu timu ambazo hazipo tena ktk ulimwengu wa soka lakini zinaonekana katika ranking; ni kama nilivyoeleza awali. Ranking ya CAF inapangwa kutokana na records ya timu. Kwa hiyo kuna timu hazipo tena katika ramani ya soka lakini rekodi zao zipo na hazijavunjwa.

CAF wanatunza rekodi kwa ushiriki wako kwenye michuano yao na record hiyo ndo wanaitumia kurank, na si uwezo wa kuchukua kombe kama wengi wanavyodhani. Watu wanajoji mbona tunaziona Majimaji kwenye list ya CAF lakini Azam haipo? Huu ni ujuha.

Huwezi kuilinganisha Azam FC ambayo haijashiriki michuano ya CAF hata mara 3 uilinganishe na Majimaji iliyoshiriki michuano hiyo karibu mara 8 na kufika hadi raundi ya pili ya kombe la washindi. Majimaji kuzorota saivi haimaanishi kuwa records zao pia zimepotea. Bado zipo na bado zitatumika kuwarank. Kama hujanielewa kariri tu kwamba rekodi za Majimaji ni nzuri kule CAF kuliko za Azam.!

Malisa GJ.!

0 comments:

Post a Comment