Dondoo muhimu kuelekea mechi za Leo ...
#Yanga vs #Al_Ahly ...
Leo club ya Yanga itaikaribisha Al Ahly katika uwanja wa taifa kwa ajili ya mechi ya kwanza Ligi ya Mabingwa .... Yanga na Al Ahly weshakutana mala 4 mpaka sasa na Al ahly imeweza kumtoa mala zote , Yanga anaonekana kuwa na matokeo mazuri akiwa ndani ya uwanja wa taifa kwani mala ya mwisho kukutana Yanga alishinda 1-0 huku mchezo wa marudiano Misri Yanga alifungwa 1-0 kisha akaja kutolewa kwenye mikwaju ya Penat (4-3 )
Kocha wa Al Ahly Maltine Jol amesema watachukua dakika 15, kusoma kasi ya wapinzani wao baada ya hapo wataanza kucheza soka lao la kushambulia kwa kutumia viungo wengi zaidi ili kuweza kujilinda na kupata matokeo mazuri wakiwa ugenini.
Kocha wa #Yanga Pluijm amesema, maandalizi yao yamekwenda vizuri na vijana wake wote wapo tayari kwa mchezo dhidi ya Al Ahly, na wamemuahidi ushindi kutokana na kukusudia kufika mbali mwaka huu kwenye michuano hiyo.
“Tulicheza nao mwaka 2014, wenyewe waliona kazi yetu ingawa walitutoa kwa panelti, lakini mwaka huu tunakutana nao tukiwa kivingine zaidi tumeimarika sana hasa safu yetu ya ushambuliaji tunawakaribisha Tanzania lakini wasitarajie kurudi na pointi Misri,”amesema Pluijm.
Kila la Kheri Yanga f.c
Leo ndio siku ukisikia Maisha bila unafiki huwa hayaendi ... Totenham vs Manchester united na West ham vs Arsenal .. Mechi hizi zinawafanya mashabiki wa Arsenal na man utd wapatane kwa muda mfupi
Man utd anataka arsenal Amfunge west ham na arsenal anaombea man utd amfunge totenhm ...
Ushindi wa Leo kwa Arsenal utamuweka katika mazingira mazuri ya kupigania Ubingwa wa ligi na vile vile matokeo ya wet ham yatamuweka mazingira mazuri ya kuingia Top 4 .. Mechi yao ya kwanza ndani ya Emirates studium Arsenal alifungwa bao 2-0 , mabao ya cheikhou kouyate ,Maoro zarate yaliweza kuacha majonzi Emiretes .
Mechi zingine za Leo ni pamoja na
Swansea City watamkaribisha Chelsea Liberty studium , mechi yao ya kwanza walitoka sare ya 2-2 ..
Manchester City atamkaribisha West Bromwich etihad studim. ...hii mechi ni muhimu kwa City ushindi wa Leo utamuweka katika mazingira mazuri ya kubaki top 4 ..
Ni hayo tu kwa Leo ..
Saturday, 9 April 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment