TOFAUTI YA KUOMBA MASTERS,
P HD KWA U LAYA NA MAREKANI, C ANADA
Ukiachilia kujumuisha mambo yote ya jumla
katika uombaji scholarship kama vile
recommendation letters, sample writing,
application nk, kuna utofauti uliopo ambao
utakusaidia kufanya maamuzi ya wapi uombe.
a) Application Fee:
Vyuo vya ulaya havina Application Fee. Hili ni
jambo muhimu sana, maana itakusaidia kuomba
vyuo vingi bure. Gharama ni za kutuma
documents kwa njia ya posta nk.
Kwa upande wa USA na Canada hii ni tofauti.
Kwa kila chuo uombacho, unatakiwa kulipa si
chini ya dola 50-100 kama fee. Hii kwa maisha
ya Kitanzania ni hela kubwa ukizingatia
unatakiwa uombe vyuo vingi ujiwekee uwezekano
wa kupata.
b) Admission Exams
TOEFL au IELTS
Kwa upande wa Ulaya, wao wana mtihani mmoja
wa English Proficiency. Unatakiwa kufanya aidha
mtihani wa TOEFL (Test of English as Foreign
Language) au IELTS (International English
Language Testing System). Huo mtihani wa
TOEFL ni wa kimarekani unafanyikia pale Chuo
cha Mwalimu Nyerere kule Kigamboni, ambapo
ada ya mtihani huo ni kama dola 185. Na mtihani
wa IELTS ni wa waingereza na hufanyikia pale
British Council ada yake ni kama laki nne hivi.
Unatakiwa kufanya mtihani mmmoja kati ya hiyo
miwili.
Kuna vyuo au nchi chache zinaruhusu applicants
kuomba vyuo bila kuonesha cheti cha Kiingereza
cha TOEFL au IELTS. Mfano, ukiomba vyuo vya
Norway wao kupitia Quota Scheme scholarship
applicants ambao wamesoma high school na
university kwa lugha ya kiingereza hawana haja
ya kuonesha/kufanya mitihani hiyo.
Ushauri wangu, usisubirie zali mpaka upate
exemption hiyo. Maana ni vyuo vichache/nchi
chache zenye kutoa exemption hiyo. Ukisubiria
zali hiyo utasubiria muda mrefu kama ukikosa
chuo husika. Ila ukifanya mtihani wa TOEFL au
IELTS utakuwa umejiongezea wigo wa kuomba
vyuo vingi, scholarships kibao ni LAZIMA uwe na
requirement hii.
Kwa upande wa USA, vyuo vyote na scholarships
zote ni lazima uoneshe cheti cha TOEFL au
IELTS. Ila sharti lingine kwa USA, kwa kila chuo
uombacho, ni lazima utumie original copy of test
results. Na ni wenye kumiliki mtihani wa TOEFL
yaani ETS ndio wenye mamlaka ya kutuma copy
ya matokeo yako ya mtihani kwenye chuo
uombacho. Na kwa kila chuo, copy ya cheti
kimoja lazima ulipie dola 15 kwa kila copy. Hivyo
ni gharama kwani ukiachilia kulipia application
fee let's say dola 70, utalipia tena dola 15 ya
TOEFL cheti kutumwa kwenye chuo. Kamwe
hawachukui copy ya matokeo toka kwako.
GRE na GMAT
Ulaya wao hawana hii mitihani ya GRE na GMAT.
Hii ni mitihani kama unataka kusoma USA only.
Mitihani hii ni kama ile matriculation enzi zile
kuingia chuoni. GRE (Graduate Record Exam) ni
kwa applicants ambao wanataka kusoma non-
management programs. Na kwa GMAT (Graduate
Management Admission Test) ni kwa wale
wanaotaka kusoma Management Programs.
Mitihani hii yote gharama yake ni kama dola 185
na inafanyikia pale kwa Mwalimu Nyerere, chuo
kikuu.
Ukiachilia gharama ya mtihani, kwa kila copy
moja utakayopata/utakayotuma kwenye chuo ni
dola 27. Kumbuka chuo chochote huku
hakichukui cheti/copy toka kwa applicant, all
results should be sent from official owners of the
exam, yaani ETS. Na hakuna chuo utakachopata
iwe ni kwa masters au PhD bila ya GRE au GMAT
exam.
Gharama unaiona: Kwa USA, kuna application fee
kati ya dola 50-100 kutegemeana na chuo, kuna
TOEFL, GRE, pamoja na gharama ya kila cheti/
copy utakayotuma kwenye chuo. Hivyo gharama
ya application ya chuo kimoja ni kama dola
100-120 kutegemeana na chuo, na bado unaweza
kukosa kwani mwombaji sio wewe peke yako.
Hivyo kiushauri, huwa ni vyema mtu kuomba vyuo
vingi vya ulaya sababu za gharama, na kama
ukiomba USA basi viwe vichache unless lengo
lako liwe ni lazima usome USA tu hivyo utaingia
gharama hizo.
Edited by Ommy Lee. 🏃🏼
Friday, 29 April 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment