Neema imezidi kuwashukia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania
wanaokipiga kwenye klabu ya TP Mazembe ya Congo DR. Baada ya Mbwana
Samatta kupata timu ya barani Ulaya hatimaye pacha wake Thomas Ulimwengu
‘Drogba wa Dodoma’ naye huenda akaungana na Samatta kwenda kuchea soka
la kulipwa barani Ulaya.
Klabu ya TP mazembe imethibitisha kupokea offer rasmi kutoka timu ya
AS Saint-Étienne inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ufaransa maarufu kama
Ligue 1.
TP Mazembe iko tayari kumwachia Ulimwengu kwenda kukipiga nchini
Ufaransa kutokana na kuondoka kwa ‘pacha wake’ Mbwana Samatta ambaye
yeye (Samatta) anaelekea nchini Ubelgiji kujiunga na klabu ya Genk
ambayo inashiriki ligi kuu nchini humo inayofahamika kwa jina la Belgian
Pro League.
Uongozi wa Mazembe umesema hauna tatizo juu ya suala hilo na uko
tayari kumwachia Ulimwengu aondoke kwasababu hatakuwa katika wakati
mzuri hasa kutokana na upweke unaotokana na kuondoka kwa Mbwana Samatta
kwenye klabu hiyo.
Samatta na Ulimwengu wamekuwa karibu sana ndani na nje ya uwanja kwa
muda wote ambao wamekuwa wakiitumikia klabu ya Mazembe, kuondoka kwa
Samatta kwenye kikosi cha Mazembe huenda kukamfanya Ulimwengu awe mpweke
(bored), ili hali hiyo isimkute Ulimwengu Mazembe wanaona ni vyema
kumruhusu aondoke kwenda kwenye klabu mpya ambapo atakutana na
changamoto mpya.
AS Saint-Étienne ipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligue 1 ikiwa
imecheza mechi 19 na kukusanya pointi 29 hadi sasa. Imeshinda mechi
tisa, imetoka sare michezo miwili na kupoteza mechi nane.
Hizo ni habari nzuri kwa Thomas Ulimwengu na kwa watanzania wote kwa
ujumla, kufanikiwa kwa nyota hao kwenda kucheza soka barani Ulaya
kutafungua fursa kwa wacheaji wengine wa kitanzania kwenda Ulaya lakini
kutaisaidia timu ya taifa ya Tanzania kutokana na uzoefu watakaoupata
kwenye timu zao za Ulaya ambapo tunaamini wao wamepiga hatua kwenye
soka.
Saturday, 2 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment