Luis Suarez alifunga bao la pili na
kuisawazishia Uruguay katika kipindi cha pili katika droo ya 2-2 dhidi
ya Brazil katika mechi yake ya kwanza ya kimataifa tangu apigwe marufuku
kwa kumng'ata mchezaji mwenzake katika kombe la dunia la mwaka 2014.
Mshambuliaji
huyo wa Barcelona alikuwa hajaichezea Uruguay katika mechi ya kimataifa
kwa takriban siku 640 kabla ya mechi ya kufuzu ya kombe la dunia siku
ya Ijumaa.
Douglas Costa aliifungia Brazil baada ya sekunde 39 kabla ya Renato Augusto kuongeza uongozi huo katika dakika ya 26.
Hatahivyo Edison Cavani aliifungia Uruguay bao la kwanza kabla ya Suarez kufunga la pili baada ya kipindi cha kwanza.
Suarez
ambaye alikiongoza kikosi hicho katika uwanja wa Itapeva Arena
Pernambuco,alimng'ata sikio mlinzi wa timu ya Italy Giorgio Chiellini
wakati wa mechi ya mwisho ya kimakundi katika kombe la dunia mnamo mwezi
Juni mwaka 2014.
Saturday, 26 March 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment