.

.

Thursday, 31 March 2016

Waungwana kila uchwao kwenye jiji hili na viunga vyake sambamba na maeneo mengi ya nchi.kuna neno wa kimataifa hulisikia likiimbwa..
Waimbaji wakuu wa neno hilo ni washabiki wa yanga wakiongozwa na mpiga zumari wao aliyeacha kazi yake na kujigeuza muimbaji.
Kinyume chake hilo neno klabu ya Simba huitwa wa mchangani au wamatopeni.wengi wananilaumu kuwa kwa nn huwa sijibu neno lolote la ajabu kwa yanga.jibu langu ni jepesi tu.lazma tujitofautishe msemaji wa klabu na mropokaji wa klabu.
Mm hupenda kuzungumzia issues sio porojo au lugha za uchochoroni.haiwezekani nikawa kiongozi kisha nikaongea lugha za mashabiki maandazi.
Kwa hyo mtaniwia radhi wapenzi wa mpira kwa kutokuwa muimbaji wa ngonjera za uchochoroni.always nitabaki msemaji wa klabu kubwa nchini na ntaongea facts kwa kadri zilivyo..

Na wadau zisomeni sifa za kimataifa kwa klabu ya Simba nje ya nchi halaf zifananisheni na timu nyingine nchini
Walau kama zitafikia nusu tunawaruhusu watafute tusi jipya.
Ombi langu kwenu isambazeni taarifa hii ktk kila mtandao wa kijamii kisha waseme wao wanaojiita wa kimataifa.

1.Simba ndio timu ya kwanza nchini kupanda ndege na hii ilikuwa mwaka 1963 tena wakati huo taifa la Tanzania halikuwa limeundwa.ilikwenda Ethiopia kwa mwaliko wa rais wa taifa hilo Haile Selassie
2,Simba ndio timu ya kwanza kuvaa jezi na hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam
3.Simba ndio timu ya kwanza kuvaa viatu nchini na hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini navy ya afrika kusini.
4,Simba ndio timu ya kwanza kuwa na basi lake yenyew na hili lilinuliwa mwaka1968.
5.Simba ndio timu ya kwanza kumiliki jengo lake lenyew na hili lilizinduliwa 1971.
6.Simba ndio timu ya kwanza kuwa bingwa wa ligi kuu nchini1966
7,Simba ndio timu ya kwanza kuwakilisha nchi na hii ilikuwa 1967.
8,Simba klabu ya kwanza nchini kwenda ulaya na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland .
9.Simba ndio timu ya kwanza kuwa mabingwa wa Afrika mashariki na kati na hii ilikuwa 1974.
10.Simba ndio mabingwa wa kihistoria wa afrika mashariki na kati.ndio timu iliochukua ubingwa mara nyingi kupita klabu yoyote afrika mashariki na kati nzima(champs off all time)
11.Simba ndio timu pekee nchini iliowahi kufika nusu fainali ya klabu bingwa afrika na hii ilikuwa1974.
12,Simba ndio timu pekee nchini na afrika mashariki kufika fainali ya kombe la caf na hii ilikuwa1993.
13.Simba ndio timu inayoshikilia rekodi afrika kama si duniani kwa kufungwa na mufurila wonderes ya Zambia goli nne kwa bila na kwenda kuibamiza tano bila kwao.mbele ya rais wao Kenneth Kaunda.hii haijafanywa na klabu yoyote afrika na nna mashaka duniani.hii ilikuwa 1979.
14.Simba ilicheza ktk hatua ya makundi ya klabu bingwa afrika 2003 kwa mafanikio makubwa kulinganisha na timu yoyote nchini.
15,Simba ndio timu pekee kuivua ubingwa klabu bingwa afrika nadi zamalek hii ilikuwa pia 2003.
16.Simba ndio klabu pekee nchini kuzifunga timu zote za mataifa ya kiarabu.kuanzia
1.waliowatoa mwaka jana etoile du sahel.Tunisia
2,widad Casablanca ya Morocco
3.el setif Algeria
4.el harach Algeria
5.halaf tumezifunga timu zote kubwa za misri.zamalek.al ahly.Arab contractors. Ismailia.mehala al kubra na timu nyingine mnajua huwa inafanywaje ikigusa kule.
6.pia imeshaitoa el merekh ya Sudan 1994 ktk klabu bingwa ya afrika.
7.Simba pia imeshazifunga miamba ya afrika ya afrika magharibi.kuanzia asec.asante kotoko.hafia ya guinea.na hata mabingwa wa kihistoria wa Zambia nkana red devils.
17.tukirudi juu Simba ndio timu ya kwanza kuvaa suti na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland.
18.Simba ndio klabu pekee nchini kujenga jengo lake lenyew kwa nguvu za wanachama na washabiki.wenzetu ni mkopo na msaada toka kwa mzee karume100%,Simba ilipewa kiasi flan na mzee karume baada ya jengo kukamilika na hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya sabini.
19.angalia idadi ya wachezaji wa Simba walioenda ulaya kucheza soka la kulipwa.
Nico njohole
Deo njohole
Kassim matitu
George kulagwa
Huku ikiwa na makumi ya nyota wake kadhaa waliowah kutapakaa sehem mbali mbali duniani.
Nikutajie wachache.
Khalid abeid
Haidar abeid
Martin kikwa
Athman mambosasa
Zamoyoni mogella
Hamis gaga
Lilla shomari
Iddi pazi
Kiwelu mussa
George masatu
Hussein masha na wengine wengi.bila kumsahau nguli wa sasa mbwana samata.mutoto ya msimbazi.
Na hapa kumbukumbu ikae vzuri wazee wangu mm Sunday na kassim manara wakati wanaenda kucheza ulaya hawakuwa wachezaji wa yanga.walikuwa wakicheza pan African.
20.nimalizie kwa kuwaambia FIFA ilizitaja timu bora za karne kwa kila nchi.kwa Tanzania Simba ilitajwa ndio timu bora ya karne na wenye mpira wao FIFA.
Nenda kwenye rekodi za caf ndio utajua nani wa kimataifa baina ya cc na wao.
Porojo za mjini ntakuwa nimezimaliza sasa.na anayebisha abishe kwa data.
Wakoloni wetu walitufundisha hv...
No reaserch no data no right to speak.tafsiri isio rasmi.hujafanya utafiti na huna takwimu funga bakuli lako.
Asanteni na nendeni mkawaambie.
Haji S Manara
Msemaji wa klabu bora ya muda wote Tanzania (best club of all time)
Ukiona errors zipotezee jadili issues na nnaruhusu challenges kama zipo
Porojo peleka kuleeeeeee..

Adiosssssssss

0 comments:

Post a Comment