.

.

Saturday, 31 October 2015

Mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza.KIVUMBI cha Ligi Kuu Tanzania Bara, kinaendelea tena leo kwenye viwanja vitano tofauti, huku miamba ya soka Yanga na Simba ikirejea tena kusaka pointi tatu. Yanga ambayo kabla ya mechi ya Jumatano iliyotoka sare ya mabao 2-2 na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage Shinyanga ilikuwa na pointi 19 sawa na Azam FC ikiongoza ligi hiyo, ilijikuta ikipata matokeo hayo ambayo yaliwapa majonzi mashabiki wao.
Majonzi hayo yaliongezeka zaidi Alhamisi baada ya Azam kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, hivyo Azam kuipiku Yanga kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 22 ikiiacha Yanga nafasi ya pili na pointi zake 20.
Kutokana na hali hiyo, leo Yanga itashuka Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora kuivaa Kagera Sugar, ikiwa na dhamira moja ya kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo. Kama Yanga ikishinda leo itafikisha pointi 23 na itaombea Azam FC ambayo kesho itacheza na Toto Africans Uwanja wa Azam Chamazi ipate matokeo mabovu.
Yanga inapewa nafasi ya kushinda leo kutokana na mwenendo mbaya wa wenyeji wao Kagera Sugar, ambao tangu kuanza msimu huu wameshinda mchezo mmoja na kupoteza mitano kati ya tisa waliyocheza.
Leo utakuwa mtihani wa pili kwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mohammed Adolf Rishard, tangu akabidhiwe timu akirithi mikoba ya Mbwana Makatta aliyeachia ngazi kutokana na matokeo mabaya. Ni wazi Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm naye ataingia uwanjani kuhakikisha vijana wake wanaibuka na ushindi ili kuwapa furaha mashabiki wao.
Hata hivyo pamoja na mwanzo mbaya wa Kagera Sugar, lakini timu hiyo inaweza kuzinduka na kufanya maajabu kwa kuifunga Yanga, kwani inakikosi bora cha wachezaji waliodumu kwa muda mrefu na timu hiyo akiwemo nahodha wake George Kavila na Paul Ngwai.
Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikizidi kujivunia safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Mzimbabwe, Donald Ngoma mwenye mabao saba na Amissi Tambwe ambao wamekuwa wakipambana kuhakikisha timu yao inafanya vizuri kwa kufunga mabao mengi.
Kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Simba inawakaribisha Majimaji ya Songea huku kocha wake Dylan Kerr, akijivunia ushindi wa bao 1-0, walioupata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga na timu hiyo kufikisha pointi 18 na kupanda hadi nafasi ya nne.
Mshambuliaji Hamisi Kiiza amekuwa tegemeo kwa kocha Kerr, katika upande wa mabao baada ya kufunga bao lake la sita Jumatano iliyopita ukiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu kurejea uwanjani baada ya kukosa mechi tatu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Pamoja na kuonesha kiwango cha chini kwenye mchezo uliopita, lakini Simba wanapewa nafasi ya kushinda mchezo wa leo kutokana na udhaifu wa wapinzani wao Majimaji waliopo nafasi ya 10 wakiwa na pointi 11.
Rekodi zinaonesha Majimaji imekuwa hatari msimu huu inapocheza nyumbani uwanja wa Majimaji Songea, lakini mambo huwa tofauti inapokuwa ugenini na takwimu zinaonesha imepoteza mchezo mmoja nyumbani na kushinda mitatu, huku ikifungwa michezo mitatu na miwili ikitoka sare.
Mechi nyingine za leo, Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo, itakuwa nyumbani Uwanja wa Manungu kucheza na Mwadui FC ya Shinyanga na Prisons itakuwa nyumbani Uwanja wa Sokoine kuchuana na Ndanda FC ya Mtwara na Coastal Union itakuwa Uwanja wa Mkwakwani ikicheza na Mbeya City.

Kiongozi wa timu ya waangalizi wa Jumuiya ya EAC katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, Moody Awori akizungumza na wajumbe wa Jumuiya hiyo mjini Dar es Salaam.WAANGALIZI kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameelezea kushangazwa na amani na utulivu uliokuwepo wakati wa kupiga kura. Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka EAC, Moody Awori, ambaye pia ni Makamu wa Rais mstaafu wa Kenya amemueleza hayo Rais Jakaya Kikwete alipofika Ikulu jana mchana.
“Sisi kutoka Kenya tulishangaa, unakwenda kwenye kituo watu wako kimya, tunakupongeza pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM),” alisema Awori. Aliongeza kuwa, “Tunatarajia kuwa uongozi mpya unaoingia madarakani, utafuata nyayo zako.”
Awori alimueleza Rais kuwa katika shughuli zao za uangalizi, walitembelea vituo zaidi ya 12 kwa siku jijini Dar es Salaam na kote hali ilikuwa shwari. Alieleza kuwa wamejifunza kitu kikubwa katika uchaguzi huo.
Watanzania kwa jadi yao ni watu wa amani na utulivu, lakini pia kabla ya uchaguzi, Rais Kikwete aliweka wazi kuwa Serikali yake ina wajibu wa kulinda watu na mali zao na kuhakikisha watu wote wanashiriki katika kupata haki yao ya kupiga kura kwa amani, uhuru na utulivu bila kubughudhiwa na hilo ndiyo jambo kubwa na la msingi kwa Serikali yake.
Awali jana asubuhi, Rais Kikwete alihudhuria hafla ya kukabidhiwa vyeti kwa washindi wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Rais mteule Dk John Magufuli na Makamu wa Rais mteule, Mama Samia Suluhu Hassan.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali na viongozi wa waangalizi wa uchaguzi hapa nchini, viongozi wa dini na watu mbalimbali. Baadaye Rais Kikwete aliongoza mapokezi ya Rais mteule katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba, ambako wanachama, mashabiki na wapenzi wa CCM walifika kumpokea na kumsalimia mgombea wao, ambaye ameibuka mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Friday, 30 October 2015

KOCHA wa Yanga Hans van der Pluijm, ameitupia lawama safu yake ya ulinzi kwa kusema ilikosa umakini na kusababisha wapinzani wao Mwadui FC kusawazisha bao la pili dakika za mwisho.
Yanga juzi ilikuwa ugenini Uwanja wa Kambarage Shinyanga kupambana na Mwadui FC, na kulazimishwa sare ya 2-2, matokeo ambayo yameiweka rehani nafasi yake ya kuongoza ligi hiyo.
Akizungumza na gazeti hili Pluijm, alisema safu yake ya ulinzi iliwanyima pointi tatu kwenye mchezo huo kitu ambacho kinaweza kuwagharimu kutokana na ushindani mkali uliopo kati yao na wapinzani wao Azam FC.
“Hatukucheza kwenye kiwango chetu cha kawaida, lakini tulistahili ushindi kutokana na namna ambavyo wachezaji wangu walivyocheza kwa kujitolea na kupata mabao yale mawili.
“Hata hivyo safu yetu ya ulinzi ilituangusha kwa kuruhusu bao la kusawazisha la dakika za mwisho,” alisema Pluijm. Mholanzi huyo alisema matokeo hayo siyo mabaya, lakini wanalazimika kupambana kwenye mchezo wao unaokuja dhidi ya Kagera Sugar ili kurudisha wimbi lao la ushindi na kuendelea kujiwekea mazingira mazuri ya ubingwa msimu huu.
Alisema katika mchezo huo wapinzani wao Mwadui, walionekana kucheza kwa kutumia nguvu nyingi na kuwakamia, kitu ambacho kiliwasumbua wachezaji wake kushindwa kuonesha kiwango chao cha kawaida ambacho wamekuwa wakikionesha kwenye michezo iliyopita.
“Mchezo ulikuwa mgumu kwa sababu tulicheza na timu ambayo ilipania kutuvurugia mipango yetu kwa kucheza vurugu, lakini nimefurahi kupata sare hiyo kwa sababu vijana wangu walilazimika kubadilika na kuendana na hali ya mchezo ilivyokuwa,” alisema Pluijm.
Katika mchezo huo mabao ya Yanga yote mawili yalifungwa na Mzimbabwe Donald Ngoma, huku yale ya Mwadui yakifungwa na Poul Nonga na Bakari Kigodeko na kuifanya timu hiyo ya Jangwani kufikisha pointi 20 katika mechi nane ilizocheza msimu huu.

DAKTARI wa Kemia, John Pombe Joseph Magufuli ndiye Rais wa Tano wa Tanzania.
Jana ambapo alitimiza miaka 56 ya kuzaliwa kwake, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilimtangaza kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Urais mwaka 2015, uliofanyika Jumapili iliyopita.
Mbunge huyo wa Chato kwa miaka 20, aliyezaliwa Oktoba 29, 1959, ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 8,882,935, sawa na asilimia 58.46 ya kura halali zilizopigwa Jumapili, hivyo kumrithi Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ya Magogoni ambayo tayari imeshakaliwa na Watanzania wengine wanne.
Mbali ya Rais Kikwete, marais wengine waliowahi kuiongoza Tanzania ni Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, ambao wameshika madaraka hayo ya juu ya nchi tangu Uhuru wa mwaka 1961.
Akitangaza matokeo hayo jana kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNCC), Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema Dk Magufuli ameshinda nafasi hiyo baada ya kujikusanyia kura 8,882,935 ambayo sawa na asilimia 58.46 ya kura halali zilizopigwa.
“Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 Ibara ya 41 (6) mgombea yeyote wa kiti cha urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais, iwapo tu amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote. Na Ibara ya 47 (ii) inasema mgombea urais akichaguliwa kuwa mshindi, basi mgombea mwenza atatangazwa kuwa Makamu wa Rais,” alisema Jaji Lubuva.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Kifungu wa 35 (e) na 35 (f) na Kifungu cha 81 (b) vya Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343, namtangaza John Magufuli kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa mwaka 2015 na pia namtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais.” Kwa msingi huo, Mgombea Mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan atakuwa Makamu wa Rais, akiwa ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo Tanzania tangu nchi ilipoundwa.
Dk Magufuli alifuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyeungwa mkono na vyama vinne vya upinzani (Ukawa), Edward Lowassa aliyepata kura 6,072,848, sawa na asilimia 39.97 ya kura halali zilizopigwa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Kombwey, katika uchaguzi wa mwaka huu, wapiga kura 23,161,440 walijiandikisha na waliopiga kura ni 15,589,639, ambayo ni asilimia 67.31 ya waliojiandikisha.
Kombwey alisema kura halali ni 15,193,862 ambayo ni asilimia 97.46 na kura zilizokataliwa ni 402,248 ambayo ni asilimia 2.58. Katika uchaguzi huo, ambao wagombea wa urais walikuwa wanane, mwanamke pekee, Anna Mgwhira wa chama kipya cha ACT-Wazalendo alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 98,763 sawa na asilimia 0.65.
Wagombea wengine kura walizopata na asilimia kwenye mabano ni Chief Lutalosa Yemba wa ADC kura 66,049 (asilimia 0.43), Hashim Rungwe wa Chaumma kura 49,256 (asilimia 0.32), Janken Kasambala wa NRA kura 8,028 (asilimia 0.05), Macmillan Lyimo wa TLP kura 8,198 (asilimia 0.05), Fahmi Dovutwa wa UPDP kura 7,785 (0.05%).
Katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2010, mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete alishinda uchaguzi huo akiwa amepata asilimia 61.17 baada ya kupata kura zaidi ya milioni 5.27 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema, Dk Willbrod Slaa aliyepata kura ya zaidi ya milioni 2.27.
Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata kura 697,014, Peter Mziray alipata kura 96,932, Rungwe aliyegombea kwa tiketi ya NCCRMageuzi alipata kura 26,321, Mutamwega Mughwaya wa TLP alipata kura 17,434 na Dovutwa alipata kura 13,123. Ujumlishwaji wa matokeo ulishuhudiwa na mawakala wa vyama mbalimbali, waangalizi, Polisi pamoja na wananchi wa kawaida, pamoja na kuhakiki matokeo hayo.
Hata hivyo, vyama viwili kati ya vinane vilivyoshiriki uchaguzi havikusaini matokeo hayo ambavyo ni Chadema na Chaumma. Chadema katika majumuisho, wakala wake Goodluck ole Medeye, waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Nne aliyemfuata swahiba wake Lowassa katika Chadema, ambaye alikuwepo wakati wa kutangaza matokeo ya majimbo, hakuwepo wakati wa kujumuisha na kusaini matokeo huku wakala wa Chaumma akigoma kusaini.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Kombwey alisema pamoja na mawakala hao kugoma kusaini hakuzuii, Tume kutangaza matokeo ya uchaguzi. Kwa mujibu wa Kombwey, Rais mteule Dk Magufuli atakabidhiwa cheti cha ushindi leo kwenye Viwanja vya Diamond Jubilee, Dar es Salaam pamoja na Makamu wa Rais, Samia.
Dakika chache kabla ya Dk Magufuli kutangazwa na NEC baada ya kumaliza kujumuisha matokeo, ambayo yalianza kutangazwa kwa umma kuanzia Jumatatu asubuhi, Rais Kikwete aliweka picha ya Magufuli katika akaunti yake ya Twitter na kuandika, “Amiri Jeshi Mkuu mpya wa Tanzania, chaguo la Watanzania, Rais John Pombe Magufuli.”
Aidha, mgombea wa ACT – Wazalendo, Anna Mghwira alimpigia simu Dk Magufuli muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi na kumpongeza, huku Dk Magufuli akimshukuru na kumwita mkomavu wa siasa na mwanademokrasia wa mfano.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, baada ya kupiga kura kijijini kwake Msoga wilayani Bagamoyo, ataondoka madarakani kwa mujibu wa Katiba Alhamisi ya Novemba 5, mwaka huu, siku ambayo Dk Magufuli atakula kiapo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuiongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo.
Dk Magufuli ambaye ni Waziri wa Ujenzi, atakuwa Rais wa kwanza wa Tanzania ambaye ni mwanasayansi, na pia mwalimu wa tatu kukaa Ikulu ya Magogoni, akitanguliwa na walimu wenzake Mwalimu Nyerere na Alhaj Mwinyi.
Amewahi kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Sengerema mkoani Mwanza akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati, na baadaye kufanya kazi katika Chama cha Ushirika cha Nyanza jijini Mwanza akiwa Mkemia.
Alijitosa katika siasa ambako alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki mkoani Kagera (wakati huo sasa Chato mkoani Geita) mwaka 1995. Amekuwa mbunge wa jimbo hilo hadi Juni mwaka huu, alipojitosa katika mchakato wa kuwania urais. Aliteuliwa na Rais Mkapa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2005. Baadaye alikuwa Waziri kamili wa wizara hiyo.
Chini ya Rais Kikwete, amewahi kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kabla ya kumrejesha Ujenzi. Dk Magufuli anasifika kwa uchapakazi na weledi katika kazi zote, alizokabidhiwa akiwa serikalini na wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kaulimbiu yake ilikuwa “Hapa Kazi Tu”.
Kaulimbiu hiyo ilimbeba na kumpambanua na wagombea wengine saba, huku akiahidi kuwa Tanzania itakuwa nchi ya viwanda chini ya uongozi wake. Katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa pengine kuliko chaguzi nyingine nne za mfumo wa vyama vingi ulioanzishwa mwaka 1992, Dk Magufuli aliendesha kampeni zake, akijipambanua kuwa ni mtu atakayeleta mabadiliko ya kweli katika utendaji wa serikali.
Aliwaahidi Watanzania kwamba atasimamia mabadiliko hayo katika kila sekta, akisisitiza zaidi maendeleo ya viwanda hasa katika kuiwezesha Tanzania kuingia kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Akifunga kampeni zake jijini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Dk Magufuli alisema amepokea ushauri kutoka kwa wananchi kwa njia mbalimbali, kutoka facebook, tweeter, mabango, vikao mbalimbali na hata ujumbe mfupi wa simu ambapo alisema imeonekana kero kubwa ni maji.
Kero nyingine alizoahidi kushughulikia ni ya nishati ya umeme, kulinda Muungano, kuendeleza ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wake, kuimarisha kilimo, uvuvi na ufugaji kwa kuboresha bei ya mazao ya kazi hizo na kuimarisha viwanda, viongeze thamani ya mazao hayo.
Aliahidi kuhakikisha kila Mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata kazi yenye kipato kizuri, kutoa mikopo ya Sh milioni 50 kila kijiji na mtaa ya kuanzisha na kuendeleza biashara, kuhakikisha elimu inatolewa bure kuanzia awali mpaka kidato cha nne na kuwashughulikia mafisadi kwa kuanzisha Mahakama ya Rushwa.
Mshindani wake wa karibu, Waziri Mkuu wa zamani, Lowassa ambaye alikuwa ndani ya CCM kabla ya kujitoa Agosti mwaka huu, aliingia Chadema na kubeba kaulimbiu ya mabadiliko, huku akiwaahidi Watanzania kuwa ataendesha serikali kwa mchakamchaka na kubadili hali ya maisha kwa Watanzania kwa muda mfupi.

TANZANIA imeandika historia mpya, ambapo jana imempata Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Dk John Pombe Magufuli, ambaye alikuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu uliohitimishwa Jumapili ya Oktoba 25, mwaka huu.
Dk Magufuli ambaye katika kampeni ya kuwania urais alikuwa na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu, si mgeni katika safu za uongozi wa Tanzania kwa kuwa amekuwa serikalini kwa miaka 20, akishika majukumu mbalimbali ambayo yalitumiwa na Watanzania kumpima.
Moja ya sifa yake kubwa tangu alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia chama hicho mwishoni mwa Mei mwaka huu, ni uadilifu katika utendaji kazi wake katika majukumu tofauti aliyokabidhiwa Rais huyo mteule wa Awamu ya Tano, anatajwa kuwa katika majukumu yote ya kitaifa aliyowahi kukabidhiwa, alionesha sifa ya juu ya uaminifu na uadilifu, ambao umeelezwa kwa namna mbili tofauti.
Ujenzi barabara Kwanza ni uongozi wake wa miradi mikubwa ya fedha nyingi, ambayo kwa muda wote wa uongozi wake hakuwahi kukumbwa na kashfa. Kwa mfano mwaka huu tu, alikuwa akiongoza Wizara ya Ujenzi, iliyokuwa na bajeti ya Sh trilioni 1.2 na Mfuko wa Barabara uliokabidhiwa zaidi ya Sh bilioni 866.
Katika miaka 15 aliyoongoza Wizara hiyo ya Ujenzi, katika ngazi hiyo alisimamia miradi ya zaidi ya Sh trilioni 9.5, lakini hakula hata senti tano, badala yake alijenga mtandao mrefu wa barabara za lami nchi nzima. Usimamizi Namna ya pili ya kuzungumzia uadilifu wake ni usimamizi wake wa watendaji na wadau wa sekta ya ujenzi, ambao amekuwa akiwapa kazi za mabilioni ya shilingi na kuisimamia kwa karibu katika kuwatumikia Watanzania.
Dk Magufuli amekuwa akisimamia makandarasi zaidi ya 8,500, wahandisi zaidi ya 15,000 na wakadiriaji majengo zaidi ya 1,300, ambao wamekuwa wakinufaika na kazi za Serikali za mabilioni ya shilingi.
Kama angetumia vibaya nafasi hiyo na angetaka kumuomba au kushinikiza kila mmoja wao ampe Sh milioni moja tu kwa mwaka, angeweza kujikusanyia pato binafsi lisilo halali la zaidi ya Sh bilioni 100 kila mwaka. Pamoja na kuwa karibu na kishawishi hicho, lakini Dk Magufuli hakushiriki kuhujumu hata senti moja na hana historia wala hakuwahi kutajwa popote kutumia vibaya nafasi yake hiyo katika sekta yenye maslahi makubwa ya kifedha.
Ukali kwa wazembe Badala ya kuomba michango ya kujinufaisha kutoka kwa wadau hao wa ujenzi, Dk Magufuli alijikuta akifukuza kazi makandarasi zaidi ya 3,000 wa ndani na nje ya nchi, bila kujali utajiri wao, pale makandarasi hao walipozembea kazi au kufanya kazi chini ya kiwango.
Namna ya tatu inayotumika kuelezea uadilifu wa Dk Magufuli, imeelezwa mara kadhaa na Jaji Joseph Warioba, ambapo alisema mwaka 1996 alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuongoza Tume ya Kero za Rushwa, alikuta sekta ya ujenzi ikinuka rushwa kubwa. Lakini, anafafanua kuwa baada ya Dk Magufuli kuanza kufanya kazi katika sekta hiyo, kelele ya rushwa katika sekta hiyo imetoweka. Uchapakazi Mbali na uadilifu, Dk Magufuli pia anatajwa kuwa mchapakazi.
Hata Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi mara kadhaa amempa jina la ‘simba wa kazi’, huku Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake, akimpa jina la ‘tingatinga’ ambalo huwa halishindwi kazi katika mazingira yoyote ya ujenzi, huku wananchi wengine wakimuita ‘jembe’. Matokeo ya uchapakazi wake, yanaonekana katika sekta ya ujenzi, alikofanya kazi kwa miaka 15 tu, ambapo amefanikiwa kusimamia ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya kilometa 17,700.
Kazi hiyo imeweka historia ambayo hata wakoloni, Wajerumani na Waingereza, waliotawala Tanganyika wakati huo tangu mwaka 1884/1885 mpaka wakati wa Uhuru mwaka 1961, zaidi ya miaka 75 walijenga mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilometa 1,360 tu. Wasifu wake Dk Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 Chato (sasa Mkoa wa Geita), hivyo jana alipotangazwa kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano, ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, ambapo alitimiza miaka 56.
Dk Magufuli ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 1991 – 1994 alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza. Mwaka 1985 – 1988 alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1981 – 1982 alisoma Diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Kati ya mwaka 1979 – 1981 alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Juu ya Sekondari Mkwawa, Iringa. Mwaka 1977 – 1978 alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza. Mwaka 1975 – 1977 alisema Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera. Mwaka 1967 – 1974 alisoma Shule ya Msingi, Chato. Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mpwapwa mkoani Dodoma.
Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha. Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma. Uzoefu wa kazi Kuanzia mwaka 2010 alikuwa Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato. Mwaka 2008 – 2010 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato). Mwaka 2005 – 2008 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
Mwaka 2000 – 2005 Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki. Mwaka 1995 – 2000 Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki. Mwaka 1989 – 1995 Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Co-operative Union (Ltd) Mwanza. Mwaka 1982 – 1983 Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati). Amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa. Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa. Mchakato wa urais Dk Magufuli alitangaza rasmi nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwishoni mwa Mei mwaka huu, baada ya CCM kutangaza rasmi ratiba ya mchakato wa urais kwa wanachama wake. Aliingia kwenye harakati za kuwania nafasi ya urais kimya kimya, tofauti na makada wengine wa CCM ambao walihutubia Taifa.
Lakini, kimya chake kiliufanya mchuano wa uchaguzi wa nafasi hiyo ndani ya CCM, uliokuwa na wagombea 42 kuwa mkali zaidi. Baada ya hapo, waliorejesha fomu walikuwa wagombea 38 na kati ya hao baada ya kujadiliwa na vikao vya juu vya Chama, ikiwemo Kamati Kuu, wagombea watano - Dk Magufuli, Bernard Membe, Dk Asha Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ally na January Makamba, ndio waliofanikiwa kupelekwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.
Baada ya Nec, ambako wagombea hao walijadiliwa na kupigiwa kura, Dk Magufuli, Balozi Amina na Dk Migiro ndio waliofanikiwa kuingia tatu bora, ambapo walifikishwa katika Mkutano Mkuu na kuomba kura na baada ya kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano huo, akapatikana Dk Magufuli kupeperusha bendera ya CCM. Ahadi zake Dk Magufuli katika mikutano yake ya kampeni, alikuwa akiahidi kushusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi aliosema atapigania kila mmoja awe na kazi ya kumpa kipato, wajenge nyumba bora.
Katika kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi ili kufikia lengo hilo, Dk Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, Serikali yake itatoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake na vijana. Mbali na kutoa mikopo hiyo izunguke katika ngazi ya kijiji na mtaa, Dk Magufuli pia alisema Serikali yake itazuia kila aina ya usumbufu, unaofanywa kwa wafanyabiashara hao, ikiwemo kukamatwa kwa bodaboda na mama ntilie.
Kwa wakulima, alisema atahakikisha pembejeo sahihi zinatolewa kwa wakati na mazao yatakayovunwa, itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa mazao yao kwa kuwa atahakikisha mbali na wakulima kupata bei nzuri ya mazao yao, watakapoiuzia Serikali itakuwa bidhaa kwa fedha taslimu. Aidha, aliahidi kuondoa ushuru unaosumbua wafanyabiashara wadogo na wakulima, ili wafanye biashara kwa uhuru wajipatie kipato halali.
Dk Magufuli pia alisema baada ya kusambaza umeme, atahakikisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vinajengwa vijijini ili kusindika mazao ya kilimo shambani ili kutoka shambani bidhaa za mazao hayo ziuzwe katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Kuhusu migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, Dk Magufuli aliahidi kukabiliana na migogoro hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa ardhi zaidi kwaajili ya wakulima na wafugaji, ili kuondoa uhaba wa ardhi uliosababisha ugomvi wa maeneo ya kulishia mifugo na kulima.
Lakini pia aliahidi kunyang’anya mashamba ambayo yamehodhiwa na watu bila kutumiwa, na kuyagawa kwa wakulima na wafugaji wasio na maeneo ya kilimo. Katika elimu, alikuwa akiahidi kuhakikisha kuanzia mwakani, wanafunzi kutoka darasa la awali mpaka kidato cha nne, wanasoma bila kulipa ada, ili kuondolea wazazi usumbufu wa watoto wao kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada.
Kwa wanafunzi wa elimu ya juu, aliwahakikishia kuwa hakutakuwa na usumbufu wa kupata mikopo na kuwataka wanahusika na kazi hiyo, kuwa tayari kwa kuwa atataka kila mwenye sifa ya kusoma elimu ya juu, apate mkopo. Katika sekta ya afya, aliahidi kujenga zahanati kwa kila kijiji na mtaa, kituo cha afya kwa kila kata na hospitali ya rufaa katika kila mkoa, na ameahidi kukomesha kero ya kukosekana dawa katika hospitali za Serikali.
Katika kero ya maji, alikuwa akisema kama amefanikiwa kujenga zaidi ya kilometa 17,700 za barabara ya lami, hatashindwa kujenga mabwawa na mtandao wa mabomba kwenda kwa wananchi ili kukomesha kero hiyo.
Pia aliahidi kujenga barabara mbalimbali za lami za kuunganisha wilaya na za mijini, huku akiahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi, ifanane na ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), taasisi aliyoianzisha na kuitetea, ambayo leo watu wengi wanatamani kuitumikia kutokana na maslahi mazuri na mafanikio yake.

Tuesday, 27 October 2015

WAKATI wakisubiri matokeo ya uchaguzi ya rais huku Tume ya Uchaguzi ikitangaza kura za wagombea wabunge na uwakilishi katika majimbo ya uchaguzi Zanzibar, Jeshi la Polisi limelazimika kuzima fujo na vurugu kutoka kwa wafuasi wa CUF waliotanda mitaa ya Mji Mkongwe na barabara kuu ya Darajani.
Vurugu zimezuka baada ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kufanya tathmini na kutangaza matokeo ya ushindi wa chama chake katika uchaguzi wa juzi kwa asilimia 52.87. Maalim Seif alitoa tathmini hiyo mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CUF Mtendeni mjini Unguja na kuitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo hayo.
Katika tathmini hiyo inaonesha kwamba mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa tiketi ya urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amepata ushindi kwa asilimia 47.13. Maalim Seif alidai matokeo waliyonayo yamekusanywa na mawakala waliopo katika vituo vya uchaguzi vilivyopo Unguja na Pemba kwa kufanya majumuisho. Hatua hiyo ilizusha shangwe na furaha kwa wafuasi wa CUF na kuanza kutembea barabarani huku gari zikipiga honi.
Baadhi ya mitaa ikiwemo Darajani na Mlandege, polisi waliweka vizuizi ambavyo vilisaidia kuwazuia wafuasi hao kuingia barabarani. Aidha, ofisi za Serikali zilizopo katika eneo la Mji Mkongwe pamoja na taasisi za kibenki, zilifungwa baada ya kuibuka kwa mazingira ya fujo na vurugu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha Jeshi la Polisi kudhibiti maeneo mbalimbali zaidi yaliyopo Mji Mkongwe pamoja na eneo la Darajani ambalo ni ngome ya upinzani.
“Tumefanikiwa kudhibiti vurugu za watu waliofanya fujo na vurugu katika maeneo mbali mbali ya mji wa Unguja na hali ni shwari kwa sasa,” alisema Mkadam. Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ni kosa la jinai kwa mtu yeyote au mgombea wa chama cha siasa kutangaza matokeo ya urais. Mapema, CCM Zanzibar ililaani kitendo kilichofanywa na Maalim Seif kujitangazia ushindi katika uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kitendo hicho ni sehemu ya vitendo na matukio ya uchochezi yanayotakiwa kudhibitiwa kwa ajili ya kuimarisha amani na utulivu. Vuai aliitaka ZEC kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu kwa mgombea huyo kwa kauli zake ambazo lengo lake kuingiza nchi katika machafuko katika kipindi hiki kigumu cha uchaguzi.
Hata hivyo, viongozi watendaji wa ZEC hawakuwa tayari kulizungumzia suala hilo, ambapo maofisa wote walikuwa wapo katika mchakato wa kupokea na kutangaza matokeo ya uchaguzi wa majimbo.

Muaniaji kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amesema kuwa dunia ingekuwa mahala salama zaidi kama tu Saddam Hussein wa Iraq na Maummar Gaddafi wa Libya wangelikuwa hai.
Bwenyenye huyo mbishi aliyasema hayo katika mahojiano na CNN baada ya kukashifu sera za kidiplomasia za rais Barrack Obama.
 
Trump alisema kuwa maafa yanayoendelea Mashariki ya Kati yalichangiwa asili mia mia moja na sera haribifu za rais Obama na bi Hillary Clinton.
''Japo tunamlaumu Maummar Gaddafi unadhani angekuwa hai magaidi wangekuwa huko ?La.'
'Angalia kwa makini hakuna Libya.'
'Libya tuliyoijua sasa imesambaratika kabisa'.
'Saddam Hussein alikuwa mtawala wa kiimla na tulijua kuwa hangeliwaruhusu magaidi kunawiri huko Iraq.'

Sasa Iraq ndio Havard ama chuo kikuu zaidi cha ugaidi duniani.
'Kama ni maswala ya ukiukaji wa haki za kibinadamu.'
'Kwa hakika hali ilivyo sasa ni mbaya zaidi kuliko tulivyodhania wakati huo.'
Bwenyenye huyo anayetarajiwa kutwaa tikiti ya kuwania urais ya chama hicho cha Republican amesema kuwa anapania kuimarisha hadhi ya Marekani.

Nahodha Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema tatizo la Simba wanaipima timu yao kwa mafanikio ya Yanga na hasa kuwa kwao kileleni, lakini wanashindwa kujua wapinzani wao wameshinda mechi zao wakiwa kwenye viwanja vipi.

johnTUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza matokeo ya awali ya urais kwa majimbo 26, yakionyesha mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli anaongoza akifuatiwa na Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Matokeo hayo yalitangazwa jijini Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva kutoka kituo kikuu cha kutangazia matokeo kilichopo katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.
MAKUNDUCHI
Akitangaza matokeo ya Jimbo la Makunduchi lililoko Zanzibar, Jaji Lubuva alisema Dk. Magufuli alipata kura 8,406 sawa na asilimia 81.20 akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, aliyepata kura 1,769 sawa na asilimia 17.9.
Katika jimbo hilo, alisema waliojiandikisha walikuwa ni 12,742 na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 10,682 sawa na asilimia 81.24.
Aliwataja wagombea wengine waliofuatia na kura zao kwenye mabano kuwa ni Hashim Rungwe – Chaumma (68), Lutalosa Yemba – ADC (58), Kasambala Marick -NRA (23) Anna Mghwira – ACT-Wazalendo (22), Macmilan Lyimo -TLP (18) na Fahmi Dovutwa – UPDP (18).

PAJE
Kwa upande wa Jimbo la Paje, Jaji Lubuva alisema Dk. Magufuli alipata kura 6,035 sawa na asilimia 81.20, Lowasa kura 1,899 sawa na asilimia 23.60 na kufuatiwa na ACT kwa kura 36.
Chaumma walipata 28, ADC kura 21, TLP na NRA kila moja kura nane na UPDP kura 7.

LULINDI
Katika Jimbo la Lulindi, Dk. Magufuli alipata kura 31,603 sawa na asilimia 71.28 na Lowassa kura 11,543 sawa na asilimia 26.03 ya kura zote halali.
Wengine ni Mghwira aliyepata kura 528, Lutalosa Yemba kura 362, Rungwe kura 179, Kasambala kura 43, Lyimo kura 45 na Dovutwa kura 34.

CHAMBANI
Jimbo la Chambani, Lowassa ameongoza kwa kupata kura 5,319 sawa na asimilia 83.90 akifuatiwa na Dk. Magufuli aliyepata kura 818 sawa na asilimia 12.90.
Rungwe alipata kura 63, Chief Yemba kura 50, Dovutwa kura 36, Kasambala kura 20, Lyimo kura 19 na Mghwira kura 15.

KIWANI
Lowassa ameongoza kwa kupata kura 4,229 sawa na asilimia 68.51 akifuatiwa na Dk. Magufuli kura 1,661 sawa na asilimia 12.9.
Mgombea wa Chaumma alipata kura 96, ADC kura 71 UPDP kura 39, NRA kura 28, ACT kura 27 na TLP kura 22.

NSIMBO
Dk. Magufuli ameongoza kwa kupata kura 31,413, Lowassa kura 6,042, mgombea wa ACT kura 183, ADC kura 64, Chaumma kura 42, UPDP kura 15, TLP kura 14 na NRA kura 6.

NDANDA
Katika jimbo hilo, Dl. Magufuli alipata kura 33,699, Lowassa kura 19,017, mgombea wa ACT- Wazalendo kura 594, ADC kura 409, Chaumma kura 189, UPDP kura 49 na TLP kura 49.

DONGE
Dk. Magufuli alipata kura 5,592, Lowassa kura 1,019, mgombea wa Chaumma kura 23, ADC kura 22, NRA kura 10, UPDP kura 7, ACT kura 5 na TLP kura 4.

KIWENGWA
Mgombea wa CCM, Dk. Magufuli alipata kura 3,317, Lowassa kura 1,104, Chaumma kura 27, ADC kura 24, TLP kura 19, ACT kura 15, UPDP kura 10 na NRA kura 9.

BUMBULI
Dk. Magufuli alipata kura 35,310, Lowassa kura 7,928, mgombea wa ACT kura 447, ADC kura 188, UPDP kura 25, NRA kura 15 na TLP kura 13.

KIBAHA MJINI
Mgombea wa CCM, Dk. Magufuli alipata kura 34,604, Lowassa kura 25,448, ACT kura 314, Chaumma kura 77, ADC kura 59, TLP kura 17, NRA kura 15 na UPDP kura 11.

MKOANI
Lowassa ameongoza kwa kupata kura 7,368, akifuatiwa na Dk. Magufuli kura 3,341, Chaumma kura 87, ADC kura 60, NRA kura 44, TLP kura 33, UPDP kura 27 na ACT kura 20.

MTAMBILE
Latika jimbo hili, mgombea wa Chadema, Lowassa amepata kura 5,875, Dk. Magufuli kura 902, Chaumma kura 56, ADC kura 41, UPDP kura 25, NRA kura 22, TLP kura 18 na ACT kura 7.
GANDO
Mgombea wa Chadema alipata kura 5,903, CCM kura 881, ACT kura 11, ADC kura 23, Chaumma kura 49, NRA kura 14, TLP 11 na UPDP 25.
MTAMBILE
Mgombea wa Chadema alipata kura 6,903, CCM kura 428, ACT kura 9, ADC kura 28, Chaumma kura 58, NRA kura12 , TLP 21 na UPDP 37.
MGOGONI
Mgombea wa CCM alipata kura 710, Chadema kura 6,506, ACT kura 12 , ADC kura 31, Chaumma kura  45, NRA kura 12, TLP  8 na UPDP 37.
KISARAWE
Mgombea wa CCM alipata kura 24,886, Chadema kura 13,093,  ACT kura235 , ADC kura 19 , Chaumma kura 314, NRA kura 26, TLP kura 22 na UPDP kura 46.
MBINGA MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 29,225, Chadema kura 11,665,  ACT kura 329, ADC kura 131 , Chaumma kura 66, NRA kura 10, TLP 16 na UPDP 16.
NANYAMBA
Mgombea wa CCM alipata kura 24904, Chadema kura 16992,  ACT kura 361 , ADC kura 202 , Chaumma kura 172, NRA kura 39, TLP 48 na UPDP 64.
MOSHI MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 28,909, Chadema kura 49,379,  ACT kura 149, ADC 186 , Chaumma kura 1,154, NRA kura 8, TLP 7 na UPDP kura 6.
MKINGA
Mgombea wa CCM alipata kura 23,798, Chadema kura 11,291, ACT kura 228, ADC kura 186, Chaumma kura 351 , NRA kura 31, TLP 29 na UPDP 27.
PERAMIHO
Mgombea wa CCM kura 32,505, Chadema kura11,291, ACT kura 359, ADC kura  135, Chaumma kura 66, NRA kura 16, TLP 15 na UPDP 22.
NJOMBE MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 33,626, Chadema kura 20,368,  ACT kura 362, ADC kura111 , Chaumma kura 78, NRA kura 14, TLP 21 na UPDP 17.
SINGIDA MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 36,035, Chadema kura 19,007, ACT kura 235, ADC kura 87, Chaumma kura 64 , NRA kura 10, TLP kura 12 na UPDP kura 7.
LINDI MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 21,088, Chadema kura 17,607, ACT kura 123, ADC kura 103 , Chaumma kura 67, NRA kura 11, TLP 6 na UPDP kura 13.
WETE
Mgombea wa CCM alipata kura 958, Chadema kura 5,119,  ACT kura 18, ADC kura 22 , Chaumma kura 28, NRA kura 15, TLP 16 na UPDP kura 10.

Tazama mikoa ambayo CCM ameitesa UKAWA. Waswahili wanasema ni shiiidah