Muaniaji kiti cha
urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amesema
kuwa dunia ingekuwa mahala salama zaidi kama tu Saddam Hussein wa Iraq
na Maummar Gaddafi wa Libya wangelikuwa hai.
Bwenyenye huyo mbishi aliyasema hayo katika mahojiano na CNN baada ya kukashifu sera za kidiplomasia za rais Barrack Obama.
''Japo tunamlaumu Maummar Gaddafi unadhani angekuwa hai magaidi wangekuwa huko ?La.'
'Angalia kwa makini hakuna Libya.'
'Libya tuliyoijua sasa imesambaratika kabisa'.
'Saddam Hussein alikuwa mtawala wa kiimla na tulijua kuwa hangeliwaruhusu magaidi kunawiri huko Iraq.'
Sasa Iraq ndio Havard ama chuo kikuu zaidi cha ugaidi duniani.
'Kama ni maswala ya ukiukaji wa haki za kibinadamu.'
'Kwa hakika hali ilivyo sasa ni mbaya zaidi kuliko tulivyodhania wakati huo.'
Bwenyenye huyo anayetarajiwa kutwaa tikiti ya kuwania urais ya chama hicho cha Republican amesema kuwa anapania kuimarisha hadhi ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment