.

.

Thursday, 6 August 2015


Wachezaji saba; Jonas Mkude, Abdi Banda, Peter Mwalyanzi, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Awadh Juma na Emmanuel Mtambuka wote hawapumui huku wakiletewa tena Mzimbabwe Justine Majabvi ambaye inaelezwa kwamba muda wowote huenda akamwaga wino Msimbazi.

SIMBA inatarajiwa kurejea leo Alhamisi jijini Dar es Salaam baada ya wiki mbili za kujifua visiwani Zanzibar, lakini tayari wachezaji wa timu hiyo hasa viungo wakiwa kwenye vita kubwa ya kuwania namba.
Ushindani mkubwa uliopo katika nafasi hiyo umewafanya wachezaji hao kuwa macho kwa hofu kwamba mtu akizubaa tu, lazima ile kwake.
Wachezaji saba; Jonas Mkude, Abdi Banda, Peter Mwalyanzi, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Awadh Juma na Emmanuel Mtambuka wote hawapumui huku wakiletewa tena Mzimbabwe Justine Majabvi ambaye inaelezwa kwamba muda wowote huenda akamwaga wino Msimbazi.
Baadhi ya wachezaji hao wamekiri kwamba ndani ya Simba kwa sasa ni amsha amsha mwanzo mwisho na hakuna kulala kwa sababu ushindani ni mkubwa na kila mmoja anapenda kumridhisha kocha, Dylan Kerr.
Mkude ambaye ni miongoni mwa wanaocheza kati sambamba na Ndemla na Mtambuka, alisema Msimbazi kwa sasa hakulaliki kwa namna ushindani ulivyoongezeka huku viungo wa pembeni Mwalyanzi na Awadh Juma ambao wanamudu vyema kucheza kwenye nafasi mbalimbali za kiungo, nao wakisema hivyo hivyo.
“Haitakuwa rahisi kwa mchezaji yeyote kupata namba kama hatojituma kwenye mazoezi, hii ni kwa sababu kila mchezaji ana hamu ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba,” alisema Mkude.
Hata hivyo jambo hilo limemfurahisha Kerr aliyesema kuwa ushindani na uwepo wa viungo wengi, unampa nafasi ya kupata ushindi kwenye kila mchezo.
“Nina viungo wengi, hii ndiyo silaha yangu ya ushindi. Kwanza nataka ushindani, lakini pia nataka niwe na uwezo wa kutumia viungo nitakavyo ninapokuwa nikitumia mifumo mbalimbali tofauti. Kama mchezo utahitaji viungo watano basi nitakuwa nao, kama ni wanne au watatu basi natakiwa kuwa nao ambao ni imara,” alisema Kerr.
VIONGOZI WATIBUA
Katika hatua nyingine, Kocha wa Viungo wa timu hiyo, Mserbia Dusan Momcilovic akichukizwa na ongezeko la wachezaji wapya kwenye kikosi chake Kerr akisema hatamwonea haya yeyote atakayeshindwa kuonesha uwezo ndani ya kipindi hiki.
Kerr alisema: “Wachezaji wanazidi kuja, sijapendekeza yeyote, lakini niko tayari kuwaangalia na ambaye hataniridhisha sitamkubali.
“Mfano ikitokea yeyote akashindwa kuonesha uwezo sitaweza kuwa naye. Nataka mchezaji mwenye kiwango kizuri, mwenye uwezo mkubwa wa kuisaidia Simba na awe wa kuitendea haki jezi ya Simba.”
1 |

0 comments:

Post a Comment