.

.

Sunday, 2 August 2015

YAMETIMIA, YA LAUDIT MAVUGO YANAFANANA NA YA MBUYU TWITE
BAADA YA MANENO YA MDA MREFU KUHUSU UJIO WA MAVUGO KATIKA KLABU YA SIMBA, HATIMAYE MCHEZAJI HUYO KUTUA KATIKA KLABU YA YANGA,
KLABU YA YANGA IMEFANIKIWA KUIZIDI UJANJA KLABU YA SIMBA KATIKA USAJILI WA MAVUGO, HAPO AWALI SIMBA ILIKUBALI KUTOA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 110 KWA AJILI YA USAJILI WA MSHAMBULIAJI HUYO KUTOKA NCHINI BURUNDI, AMBAPO GEOFREY KABURU NDIYE ALIKUWA MFUATILIAJI WA SWALA ZIMA LA USAJILI WA MAVUGO, LAKINI KLABU YA YANGA KUPITIA KWA KIGOGO WAKE WA KAMATI YA USAJILI IMETIBUA DEAL HIYO YA KLABU YA SIMBA, AMBAPO IMEFANIKIWA KUMCHUKUA MAVUGO KWA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 140, AMBAPO PIA IMELAZIMIKA KUTOA SHILINGI MILIONI 30 KWA KLABU AMBAYO ILIMLEA LAUDIT, KLABU ANAYOICHEZEA MAVUGO HIVI SASA KWA LENGO LAKUKWAMISHA MAVUGO KWENDA SIMBA ILIIAMBIA KLABU YA SIMBA KAMA INAMTAKA MAVUGO BASI ITOE SHILINGI MILIONI 200 JAMBO AMBALO LIMEKUWA GUMU KWA KLABU YA SIMBA, HII NI MARA YA PILI KWA KLABU YA SIMBA KUZIDIWA KETE NA KLABU YA YANGA KATIKA USAJILI WA WACHEZAJI WA KIMATAIFA, MAVUGO KWA SASA NDIYE KINARA WA KUPACHIKA MABAO NCHINI BURUNDI, BAADA YAKUKAMILISHA VIPIMO VYA AFYA NDANI YA KLABU YA YANGA ATAUNGANA NA MRUNDI MWENZAKE AMIS TAMBWE PAMOJA NA MSHAMBULIAJI DONARD NGOMA KUTOKA ZIMBABWE KUUNDA SAFU YA USHAMBULIAJI, MAVUGO ANACHUKUA NAFASI YA MLIBERIA KPAH SHERMAN ALIYETIMKIA NCHINI AFRIKA KUSINI

YANGA PIA IPO KATIKA MPANGO WA KUACHANA NA ANDREW COUTINHO ILI NAFASI YAKE IZIBWE NA MCHEZAJI WA KIMATAIFA WA KIUNGO CHA CHINI MWENYE UWEZO WA JUU KATIKA UKABAJI, UCHEZESHAJI WA TIMU NA UPANDISHAJI WA MASHAMBULIZI
LAKINI PIA NDANI YA KLABU YA YANGA BADO KUNA MVUTANO MKUBWA KATI YA UONGOZI NA BENCHI LA UFUNDI JUU YA NAFASI ANAYOCHEZA NA UWEZO WA MGHANA JOSEPH ZUTAH TETEH

0 comments:

Post a Comment