Katika kile kilichotafsiriwa kama dongo kwa chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA, kiongozi wa chama cha ACT Zitto Zuberi Kabwe, ameweka
maneno yanayoonesha kushangazwa na hatua ya CHADEMA kumpokea aliyekuwa
waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa.
Picha lilianza juzi usiku baada ya Zitto kupitia ukurasa wake wa
Twitter, kupost picha ya kwanza ya Lowassa akiwa na viongozi wa juu wa
CHADEMA akiipa ‘caption’ ya “mambo yanaendelea kutokea tusubiri chochote
kwenye uchaguzi mkuu Oktoba”.
Ikiwa ni masaa machache tangu Mbunge huyo wa Monduli, kukabidhiwa kadi
ya CHADEMA zito ameandika kupitia Facebook “wekeni akiba ya maneno”
akiwaacha followers wake zaidi ya 25,000, kwenye mataa wasielewe
alikusudia nini hasa.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Bazil Mbekini ameitafsiri sentensi hiyo
kama ‘makavu’ kwa CHADEMA kwa kusahau kile walichokuwa wakimuita
Lowassa fisadi, na leo wamemkaribisha kwenye chama hicho.
Uchaguzi umetafsiriwa.
Ni chaguo kati wenye misingi dhidi ya wenye uchu wa madaraka. Kati ya Maadili dhidi ya wabadhirifu. Kati ya wenye msimamo dhidi ya wanaobebwa. Utakuwa uchaguzi wenye Hamasa zaidi kupata kutokea nchini Tanzania

0 comments:
Post a Comment