WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira (pichani),
ameshinda kura za maoni za CCM, baada ya kupata kura 6,429 na kumshinda
mpinzani wake wa karibu ambaye ni mjasiriamali, Robert Maboto aliyepata
kura 6,206.
Akitangaza matokeo hayo jana katika ofisi ya CCM ya Wilaya ya Bunda,
Mkurugenzi wa uchaguzi katika wilaya hiyo, Magreth Mtatiro, alisema
Wassira alishinda kwa zaidi ya kura 223 kati ya kura zote zilizopigwa
15, 262.
Mtatiro alimtangaza mshindi wa tatu kuwa ni Mwenyekiti wa CCM mkoani
Mara, Christopher Sanya aliyepata kura 1,140, ambapo wengine ni pamoja
na Exavery Lugina aliyepata kura 846, Simon Odunga (547), Magesa Mugeta
(446), Peres Magiri (385) na Burian Bitaa (263).
Kutokana na matokeo hayo, Mtatiro alimtangaza Waziri Wasira ambaye
anatetea tena nafasi hiyo, kuwa mshindi katika kinyang’anyiro hicho cha
kura za maoni. Wakati huohuo, mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo
la Mwibara Kangi Lugola (pichani kulia), ameshinda uchaguzi katika kura
za maoni za chama hicho na kumshinda kwa kura nyingi mpinzani wake wa
karibu, Charles Kajege aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Sunday, 2 August 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment