Akitangaza uamuzi huo, Blatter (79) alisema baada
ya kuitisha mkutano wa dharula wa Fifa: ”Muda mfupi ujao kunatakiwa
kuchaguliwe rais mpya.”
Blatter alichaguliwa wiki iliyopita kuliongoza
shirikisho hilo, licha ya wajumbe saba wa juu wa Fifa kukamatwa na
maafisa usalama wa Marekani siku mbili kabla ya uchaguzi huo.
Blatter alisema: “Uamuzi huu hauungwi mkono na kila mtu.”
Awali Fifa ilikanusha madai kwamba katibu wao
mkuu, Jerome Valcke alihusika katika kashfa ya ufisadi ambapo hongo ya
mamilioni ya dola ilitolewa.
Fifa inasema hamna afisa wake yeyote wa ngazi ya juu aliyehusika kwa njia yoyote katika kashfa hiyo.
Inasemekana malipo hayo ya rushwa yalitolewa na serikali ya Afrika Kusini kwa maafisa wa soka wa huko Marekani ili waunge mkono
Awali Fifa ilikanusha madai kwamba katibu wao mkuu, Jerome
Valcke alihusika katika kashfa ya ufisadi ambapo hongo ya mamilioni ya
dola ilitolewa.
Fifa inasema hamna afisa wake yeyote wa ngazi ya juu aliyehusika kwa njia yoyote katika kashfa hiyo.
Inasemekana malipo hayo ya rushwa yalitolewa na
serikali ya Afrika Kusini kwa maafisa wa soka wa huko Marekani ili
waunge mkono wenzao Waafrika waliong’ambo katika nchi za visiwa vya
Caribbean.
Waendesha mashtaka wa Marekani wanasema hongo hiyo
ilinuiwa kusaidia kununua kura kuiwezesha Afrika Kusini kuwa mwenyeji
wa Kombe la Dunia lililofanyika mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment