KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), AbdulrahmaWIKI hii ni ya mwisho kwa watia nia ya urais wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kurejesha fomu baada ya kuzunguka nchi nzima kuomba wadhamini,
hata hivyo jana mwanachama mwingine wa CCM alichukua fomu na hivyo
kufanya idadi ya watia nia hao kufikia 42.
Kada huyo Banda Sonoko alijigamba kuwa ana uwezo wa kuipeperusha
bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu unataotarajiwa kufanyika Oktoba
mwaka huu, kwani ana vigezo, sifa na uwezo wa kuvaa viatu vya Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu
kwenye makao makuu ya chama, alisema anajiamini kuwa ana uwezo wa
kuongoza taifam jambo ambalo limemsukuma na kuamua kuchukua fomu.
Sonoko, ambaye kwa taaluma ni mwalimu, alisema ana uwezo wa kuvaa
viatu vya Baba wa Taifa, ambavyo kwa sasa wengi wanavitamani. ‘‘Kwa sasa
wengi wanatamani kuvivaa, lakini mtu pekee vinayemtosha ni mimi.”
Alisema katika uongozi wake yeye ni muumini wa muda hivyo atahakikisha
anafanya kazi ili kuiondoa nchi katika misukosuko ya kiuchumi.
Aidha aliahidi kuweka usimamizi madhubuti wa serikali yake katika
uchumi wa kilimo na kufufua viwanda ili kuhakikisha nchi inarudi katika
kilimo.
Pia alisema atahakikisha serikali yake inakusanya kodi ili nchi iweze
kujiendesha kutokana na kodi inayokusanywa. Mwisho Alhamisi Ni siku nne
zimebaki ili kufikia tamati ya kuchukua na kurudisha fomu.
Hata hivyo mgombea huyo urais hakueleza atatumia mbinu gani kwenda
angalau mikoa 15 inayotakiwa na CCM kusaka wadhamini ili aweze kukidhi
vigezo vya jina lake kujadiliwa na vikao husika.
Kila mwanachama aliyechukua fomu anatakiwa kuwa wadhamini 450 katika
mikoa 15 ambapo mitatu iwe ya Zanzibar. Waliorudisha fomu ni Waziri wa
Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal,
Makongoro Nyerere, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Kilimo
na Ushirika, Steven Wassira na Balozi Ally Karume.
Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo, Balozi Amina Salum Ally, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias
Chikawe, Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Agustino Ramadhani, Leone
Murenda, Profesa Mark Mwandosya na Boniface Ndembo.
Watia nia wazidi kujitapa Wakati hayo yakiendelea baadhi ya wagombea
urais wamezidi kujitapa mikoani ambako wanatafuta wadhamini huku
wakieleza yale ambayo wataenda kuyafanya mara watakapoteuliwa na chama
chao kugombea urais na baadaye kuchaguliwa kushika wadhifa huo.
Fadhili Abdallah anaripoti kutoka Kigoma kuwa Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na Serikali yake, haviwezi kutishwa na mtu yeyote katika
kutekeleza maamuzi yoyote kutokana na kuwa na historia ya kuwa na
msimamo usioyumba na uongozi thabiti.
Membe, ambaye ni miongoni mwa wana CCM waliotangaza nia ya kuwania
urais kupitia chama hicho, amesema yeye binafsi hatokuwa na kinyongo kwa
maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na chama hicho hata ikiwa yatakuwa
maamuzi machungu kwake.
Akizungumza na wanachama wa CCM wa mkoa wa Kigoma waliofika
kumdhamini juzi Jumamosi, Membe alisema Watanzania wakatae vitisho na
ulaghai kutoka kwa mtu yeyote katika maandalizi ya uchaguzi Mkuu wa
mwaka huu.
“Watanzania tukatae aina yoyote ya vitisho wala ulaghai katika
uchaguzi wetu. Sisi na wengine katika makundi yetu tutakaa kusubiri
maamuzi sahihi ya chama chetu, ambacho hakikufanya makosa miaka yote ya
nyuma… “Tutaheshimu maamuzi yatakayotoka Dodoma siku ile hata yangekuwa
machungu kama pilipili.
Na ole wao ama ole wake mtu yeyote atakayejitia kuletaleta bughudha
pale eti kwa kisingizio kwamba eti chama hakikuchukua hatua sahihi,
mtachukua hatua sahihi maana mna uzoefu wa kufanya hivyo.
“Ndugu zangu Watanzania kataeni upuuzi wa aina hiyo, angalieni vigezo
mkiangalia familia zenu kwamba na kuhoji kama nikimpa huyu kesho
nitakuwa salama!” Alisema Membe huku akishangiliwa na wana CCM
waliokuwapo.
Alisema ni wajibu wa wana CCM kumpa uongozi ambaye wakiangalia
watakuwa na imani kwamba nchi na familia zao zitakuwa salama na heshima
na amani ya nchi itakuwa katika mikono salama na si vinginevyo.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya Kigoma alikomalizia mkoa wa 31,
Membe alisema ataimarisha miundombinu ya reli na barabara na kuwasaidia
kupata mwekezaji atakeyefanikisha mpango huo.
Alisema kampuni moja ya Kichina imeonesha nia ya kuboresha huduma ya
reli ikiwa ni pamoja na kujenga reli ya kisasa kati ya Dar es Salaam na
Kigoma ambayo itawezesha safari ya siku moja.
Membe, ambaye amekuwa akiahidi kusimamia uchumi wa viwanda
unaotegemea kilimo, alisema viongozi waliotangulia akiwamo Rais Ali
Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na sasa Jakaya Kikwete, wameweka misingi
imara katika maendeleo, na hivyo itakuwa ni rahisi kwake kuendeleza
walipoishia.
Jana alipokuwa Sumbawanga na Mpanda, alimsifia Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda ambaye alisema ni mmoja wa watangaza nia mwenye sifa za kuwa
kiongozi wa nchi kutokana na historia yake ya uadilifu ndani na nje ya
serikali na kwamba ingekuwa si mwanasiasa huyo angekwisha kujiona mteule
ndani ya CCM.
Makamba Naye John Mhala anaripoti kuwa Mgombea urais kupitia
CCM,Januari Makamba amesema anaamini kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kitawaletea Watanzania mgombea urais atayekubalika mbele ya wananchi
wote na sio vinginevyo.
Kauli hiyo alisema hayo katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha mara
baada ya kupata wadhamini 2,237 waliojitokeza kumdhamini nafasi hiyo
ndani ya chama.
Makamba alisema CCM haiwezi kuteua mgombea ambaye hakubaliki na
wananchi kamwe; bali itamteua mgombea wake ambaye anakubalika na
wananchi na watamkubali kwa asilimia kubwa.
Alisema kwa sasa Watanzania wanataka mabadiliko ndani ya chama na
mabadiliko hayo ni kumtaka mgombea mpya mwenye mtazamo mpya na malengo
mapya kwa maslahi ya nchi sio wale wale wa miaka yote.
Makamba ambaye alikuwa akihutubia kwa umakini mkubwa, alinukuu hotuba
ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ya mwaka 1995 katika mkutano
mkuu wa chama ambapo alisema kuwa nanukuu, Alisema kutokana na hali hiyo
chama kitafanya mabadiliko ndani ya chama kwa kumteua yeye kuwa mgombea
urais kwani Watanzania wana imani naye kwa kuwa atakuwa na mambo mapya
na mitazamo mipaya ya kuiongoza nchi hii.
Akizungumza ajira kwa vijana alisema Mkoa wa Arusha una vitu vingi
kwa vijana kupata ajira akiwemo Utalii, madini, viwanda, kilimo na
biashara ndogo ndogo na kusema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa mgombea
urais ana uhakika wa kubuni mambo mapya kwa vijana kupata kupitia vitu
hivyovitano.
Tuesday, 30 June 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment