MKULIMA kutoka Kasulu mkoani Kigoma, Eldeforce Bilohe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchuk MKULIMA kutoka Kasulu mkoani Kigoma, Eldeforce Bilohe (43) jana
alichukua fomu za kuwania urais na kusema kuwa kati ya wagombea 27 ambao
wamejitokeza haoni kama kuna mgombea ambaye ni tishio kwake.
“Kati ya wagombea 27 ambao tayari wamechukua fomu kabla yangu sioni
kama kuna mgombea tishio kwangu,” alisema mgombea huyo huku
akishangiliwa.
Bilohe alifika ofisi za makao makuu ya CCM saa nane mchana ambapo
alilakiwa kwa shangwe na vigelegele na watumishi wa CCM makao makuu.
Hata hivyo, alishindwa kueleza vipaumbele vyake mpaka anamaliza muda
wa kujieleza. Mgombea huyo ambaye alisahau kuzima simu yake wakati
akizungumza simu hiyo ikaita na kuamua kuipokea.
“Subiri kidogo,” aliongea na simu kisha akakata. Akizungumza juu ya
azma yake, alisema ameamua kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwani amekuwa na dhamira hiyo tangu mwaka 2003.
“Dhamira hiyo iko moyoni tangu mwaka 2003 pale ambapo nilipotaka
kuweka mambo sawa baadhi ya mambo yalijitokeza na kuchelewesha kusudio
hilo,” alisema.
Alisema ilipofika mwaka 2015 aliamua kurudia nia yake ya dhati na
Februari 5, mwaka huu alitangaza azma hiyo kwenye gazeti ya Sauti Huru.
“Ninaomba kutafutiwa wadhamini kila mkoa ili kusaidiana nani kufika
Dodoma kuomba kuteuliwa na CCM.”
Alisema kabla ya kuchukua uamuzi huo aliuliza baadhi ya watu ambao
baadaye walimshauri agombee nafasi hiyo. “Nikafuata utaratibu baadae
wakaniambia nikagombea, nikaenda kwa mwenyekiti akaniuliza je utaweza,
nikamjibu nitaweza nikamwambia cha msingi ni kuniweka kwenye sala,”
alisema.
Alisema wakati akijiandaa kufika Dodoma likajitokeza suala la
kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ikabidi amalize
zoezi hilo.
“Ilipofika Juni 3, mwaka huu nikawaomba barua ya kwenda Dodoma
wakalifanyia kazi suala hilo, nikafika CCM mkoa wakakubali.” Alisema
elimu yake ni ya taifa (darasa la saba) na amefika Dodoma kuchukua fomu
za kugombea Urais akiwa kama Mtanzania “Nimekuja kama Mtanzania sikuja
kama mchezo wa kupoteza fedha zangu”.
Alisema fedha za kuchukua fomu zimetoka mfukoni mwake na hajachangiwa
na yeyote. Alipoulizwa kwa nini hajaongozana na mkewe alisema kwa
sababu ambazo hazijaweza kuzuilika, mkewe alimtaka atangulie lakini pale
atakapohitajika atapatikana.
Alipohojiwa kwa nini hana vipaumbele kutokana na nafasi anayogombea
kuwa ni nyeti alisema ajira kwa vijana na maisha bora kwa wastaafu.
Juzi mgombea huyo alitinga makao makuu ya CCM kuchukua fomu ya kuomba
ridhaa kuteuliwa kuwa mgombea bila kuwa na ada, jambo ambalo lilifanya
zoezi lake la kuchukua fomu kuahirishwa.
Mjasiriamali naye ajitosa Mkazi wa Kata ya Mwisenge Wilaya ya Musoma
mkoani Mara, Boniface Ndengo (40), jana alichukua fomu ya kuwania Urais
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema ameamua kuchukua fomu ili kutimiza azma yake ya kutumikia
wananchi. Ndengo ambaye mtaalamu wa masuala ya biashara na uongozi,
alisema watu wanafanya siasa kama mambo ya kubahatisha bahatisha tu,
lakini siasa ni taaluma inayoshughulika na kuboresha maisha ya watu na
ana majukummu makubwa ya kushughulikia.
Pia alisema amekuwa akishangazwa kuona watu wenye umri mkubwa
wakitafuta madaraka makubwa ya kutumikia wananchi wakati wakiwa
wamechoka.
Alisema mtu anapofikia umri wa kustaafu anatakiwa kupunzika na si
kutafuta kufanya shughuli za kisiasa. Alisema uongozi unatakiwa kufanywa
na watu wenye umri wenye nguvu na si wenye umri wa kustaafu.
“Ni jambo la kujiuliza kwa nini kazi ya Urais inatafutwa na watu
wenye umri wa kustaafu kwani umri wao umeshakuwa mkubwa na watu
wameshachoka na wanatakiwa kupumzika,” alisema.
Alisema mahitaji makubwa ya Watanzania ni kupata kiongozi wa nchi
atakayeweza kuondokana na umaskini. Alisema akiwa kama mtaalamu wa
masuala ya biashara na uongozi na moja wa wahitimu wenye ufaulu bora
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amekuwa mbunifu wa mifumo mbalimbali
ya kufaulisha sekta binafsi.
Alisema kutokana na taaluma hizo ameona ni wakati muafaka kwake
kuwashawishi Watanzania kumpa fursa kutekeleza jukumu kubwa la nchi
ilikusaidia watanzania kutoka kwenye umaskini.
Thursday, 11 June 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment