.

.

Thursday, 18 June 2015

Tangu uondoke mengi yamejiri huku,naomba nikujuze kidogo angalau japo upate chochote
kuelekea UCHAGUZI mkuu 2015,
Tuna wasapika ki Richmond Richmond,
Tuna facebukika ki Escrow Escrow,
Tuna twitika ki Dowans Dowans,
Tuna instagramika ki Symbion symbion,
Tuna gugika ki meremeta meremeta,
Tuna extrimika kutangaza nia,
Tunafurushika kuomba ridhaa Ikulu
Mwalimu hivi si ulisema IKULU si pango la wanyan'ganyi???basi huku watangaza tamaa wanakaribia kuvuka hata idadi ya wabunge wa chama chako cha CCM,
Mwalimu nakumbuka sana uliagiza kila Waziri awe anasoma kitabu cha mchumi kilimo wa kifaransa Rene Dumont, cha Africa inakwenda pabaya (false start in Africa),ili kujua changamoto za kiuchumi na namna ya kuzitatua
Sasa hivi thubutu kila kitu ni watsapp,kila kitu ni Instagram, watu wanapiga picha kaburi lako wanapost tu watsapp,tweeter, Facebook eti wanakuenzi,wakitoka butiama eti wanatangaza nia umewapa baraka mwalimu ni kweli????kwa nini wasienzi Azimio la Arusha
Mwalimu uadilifu uliotufunza leo haupo tena
Mwalimu kumbuka uteuzi wa uwaziri mkuu mwaka 1984 baada ya kifo cha sokoine,Pamoja na hayati Paul Bomani,nafasi kubwa ilikua kwa John samwel malecela
Mwalimu ulifanya maamuzi magumu,yakumuengua Malecela kwa sababu ya kauli yake ya dharau kwa wananchi,waliolalamikia ufanisi duni wa shirika la Reli,chini ya wizara yake aliwaambia wananchi "waende Kuzimu"
Mwalimu huku Leo hii wanawasapika wa Escrow tukiwahoji tunatukanwa "ni pesa ya mboga" wengine "vijisenti tu"
halafu wengine wanafesibukika kirichmonde monde ukiwahoja wanajibu SAFARI YA MATUMAINI and of course natural justice,na wengi hatujasoma hatuelewi kama ni matusi au laah,
Mwalimu huku kwa sasa watu wana timu,na upinzani umeanzia CCM,kuna TIMU RICHIMONDEKA,kuna TIMU MAKUFURI YA POMBE,kuna TIMU MIEMBENI,kuna timu FEBRUARY MANYUZI,kuna TIMU MIHOGO,kuna TIMU MIZENGWE,kuna TIMU MAUGOKO NYENYERE,na zingine nyingi zinajisajili duuuuuh
Mwalimu wengine tunahisi Chama kimekosa meno,hakina taratibu sijui,hakina washauri sijui,hakina sheria na taratibu sijui,hakina kamati ya maadili sijui,yaani tuna SIJUI SIJUI milioni moja na ushehe
Mwalimu hivi si ulisema UTUMWA wa NCHI uliokomesha,tena na nyimbo tuliimba???
Mmmh sasa huku kuna utumwa mpya wa fikra watu wananua makundi ya ushawishi Mwalimu,watu wanauza utu wao Mwalimu,watu hawana rangi ya utaifa tena
Mwalimu, Mwalimu weeeeeh wenyewe wanamsemo wao wanasema ni shiiiiidaaaaaaah
Mwalimu kuna hawa ndugu zetu wa
UKIWA,bwana wanapiga hao,ungewapenda Sana,bungeni wanapiga mawe hao,ngumi jiwe hao,wanafanana na uzalendo hao,na ninahisi watashinda uchaguzi hao lakini je watapewa haoo?????
Mwalimu hawa vijana UKIWA bwana Mimi Nina amini ungewasapoti tu hivi Mwalimu kumbe ulikua mpinzani ndani ya chama uliyaona madudu etii eeeh????
Mwalimu au ndo mana ulikua HUVAI JEZI ZA YANGA kwanini??
OK nimeshaelewa tayari ulimaanisha chama ni itikadi za moyoni,uzalendo wa moyoni,harakati za moyoni,falsafa za moyoni,safi nimekupata
Mwalimu hawa watangaza tamaa,ooops sorry watangazania nimewashauri kabla ya kutangaza nia wakutane pale chamwino ikulu Dodoma,waweke CD za hotuba zako wakimaliza ndo watangaze nia
HIVI ni nani angetangaza nia????eti Mimi nahisi Kama DK SALIM A SALIM,MAUGOKO NYENYERE,NA WAHASIRA HASIRA STIVU,watu wanaangalia Sura eti Wahasira hasira anatisha,mmmmhhhhhhhh
HAYA MWALIMU MIMI NI HAYO TU,pumzika vizuri Mwalimu,
IJUE TANGANYIKA KWANZA KABLA TANZANIA HAIJAKUJUA
MUNGU IBARIKI TANZANIA

0 comments:

Post a Comment