KOCHA Msaidizi wa timu ya soka ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa
amesema pengo lililoachwa na winga hatari nchini, Mrisho Ngassa
litachukua muda mrefu kuzibika kutokana na uwezo binafsi aliokuwa nao.
Ngassa amejiunga na Free State inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini
PSL, kwa mkataba wa miaka minne baada ya kumaliza muda wa kuitumikia
klabu hiyo ya Jangwani kwa misimu miwili mfululizo.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mazoezi ya jana asubuhi kwenye
uwanja wa Karume Dar es Salaam, Mkwasa alisema anajua wamesajili
wachezaji wenye uwezo mkubwa na aina ya uchezaji kama Ngassa lakini siyo
rahisi wachezaji hao wakacheza kama ilivyokua kwa nyota huyo.
“Ngassa atabaki kuwa Ngassa na hiyo inatokana na aina ya uchezaji
wake na tunachotakiwa kufanya sisi kama makocha ni kuwatengeneza
wachezaji hawa tuliowasajili ili waweze kucheza kitimu na kutusaidia
lakini siyo kujifananisha na Ngassa,” alisema Mkwasa.
Kocha huyo msaidizi alisema ana matumaini makubwa na mchezaji Duesi
Kaseke waliyemsajili kutoka Mbeya City, lakini Aidha, kutakuwa na tuzo
ya kipa bora inayowaniwa na makipa Mohamed Yusup (Prisons), Said Mohamed
(Mtibwa Sugar), Shaban Kado (Coastal union).
Tuzo ya kocha bora inawaniwa na Goran Kopunovic (Simba SC), Hans Van
Der Pluijm (Yanga) na Mbwana Makata - (Prisons). Kwa upande wa mwamuzi
bora, tuzo hiyo inawaniwa na Israel Nkongo, Jonesia Rukyaa na Samwel
Mpenzu.
Tuzo ya timu yenye nidhamu inawaniwa na Mgambo JKT, Mtibwa Sugar na
Simba. Kwa mujibu wa mkataba wa Vodacom, mfungaji bora atazawadiwa Sh
milioni 5.7, sawa na kipa bora na mchezaji bora.
Timu yenye nidhamu itawazwadiwa Sh milioni 17.2, mwamuzi bora atapata Sh milioni 8.6 sawa na kocha bora.
Katika hatua nyingine, mchezaji John Mahundi wa timu ya Coastal Union
amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Mei, 2015 na jopo la makocha
kufuatia kuwazidi wachezaji wengine 14 aliokuwa akiwania nao nafasi
hiyo.
Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi huo, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu Sh milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu.
Thursday, 11 June 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment