Akizungumza kwenye makao makuu ya klabu hiyo,
Msimbazi jijini Dar es Salaam, ofisa habari wa Simba, Haji Manara
alisema klabu yao imeamua kumwaga mboga baada ya kuona inafanyiwa
hujuma.
“Sisi Simba, sasa imetosha, kama watu wanaamua
kumwaga ugali, sisi tunamwaga mboga, hatutaki kuyumbishwa,” alisema
Manara kwa jazba huku akieleza kuwa muda wa kuyumbishwa kwa klabu yao
umepita.
Hivi karibuni, Messi alihusishwa na kufanya mazungumzo ya kujiunga na Azam.
Kuhusu hilo, Manara alisema wanatafuta ushahidi ili kuishtaki klabu pinzani ambayo ilifanya mazungumzo na mchezaji huyo.
“Tumesikia kuna klabu imefanya mazungumzo na
mchezaji wetu, Messi ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja, kama
inamtaka ije tuipe dau letu, lakini si kuitana kinyemela.
Akijibu shutuma hizo, Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba
alikanusha madai ya kufanya mazungumzo na Messi na kueleza kuwa haina
mpango wa kumsajili nyota huyo wa Simba.
Sababu za kumkosa Busungu
Simba katika mchakato wa kupata saini ya
mshambuliaji Malimi Busungu wa Mgambo JKT aliyejiunga na Yanga mwishoni
mwa wiki iliyopita na kumkosa.
Hata hivyo, Manara alibainisha kuwa ilimwacha
nyota huyo ambaye alitaka fedha ambazo haziendani na thamani ya kiwango
chake uwanjani.
“Tulimwambia ukweli Busungu kuwa kama ana nia ya
kucheza Simba, dau letu ni Sh5 milioni, yeye akahitaji Sh40 milioni,
fedha ambazo tulimwambia hatuwezi kumpa kwani hajafikia kiwango hicho,”
alisema Manara.
Naye mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba,
Zacharia Hanspoppe aliwaponda Yanga kiaina baada ya kudai kuwa wao
hawataki kusajili wachezaji wanaovuma, bali wanasajili kwa kuangalia
mahitaji ya timu.
Alisema anajua kuwa wengi wanataka kuona Simba ikisajili
wachezaji wenye majina makubwa na wanaovuma hivi sasa, lakini wao
hawaangalii hilo, wanachoangalia ni ubora wa mchezaji na mahitaji ya
kikosi chao kwanza.
“Sisi wala hatutaki kushindana na mtu katika
kusajili, eti huyu kasajili huyu na sisi tusajili yule, hilo kwetu
halipo, tunachofanya ni kusajili kulingana na timu inahitaji nini kwa
wakati huo,” alisema Hanspoppe.
“Timu yetu bado ni nzuri, inakosa mambo madogo
madogo, hivyo tunachofanya ni kukiongezea nguvu katika nafasi ambazo
tumeona zimepwaya na wala hatutaki kusajili mchezaji kwa sababu jina
lake linavuma, tunasajili mchezaji tunayemhitaji na siyo anayevuma,”
alisema Hanspoppe.
Rage ahusishwa sakata la Messi
Klabu ya Simba imekuwa katika marumbano na
mshambuliaji wake, Ramadhan Singano ‘Messi’ ambaye anadai kughushiwa kwa
mkataba wake. “Mkataba wa Messi tumeurithi kwa uongozi uliopita
(mwenyekiti alikuwa Ismail Aden Rage) na walimsajili kwa mkataba wa
miaka mitatu, leo hii anadai alisaini miaka miwili. “Dole gumba na saini
ni ya Messi na tulipomuuliza alisema alisainishwa na Mzee Kinesi
(Joseph Itang’are), niweke wazi kuwa Simba haijawahi na haiwezi kughushi mikataba ya mchezaji yeyote,” alisema.
Alisema klabu hiyo imeunda kamati maalumu kuchunguza jambo hilo na itachukua hatua stahiki baada ya uchunguzi wao kukamilika.
Yamtupia virago Amri Kiemba
Akizungumzia usajili wa mchezaji Amri Kiemba
ambaye Azam aliyokuwa akiichezea kwa mkopo imeeleza dhamira ya
kumrudisha ilikomtoa (Simba), Manara alisema klabu hiyo haina mpango na
mchezaji huyo.
“Hatuna mpango wa kumrudisha Kiemba, hatuna nafasi
hiyo,” alisema Manara ambaye hakuwa tayari kuweka wazi kama mkataba wa
mchezaji huyo na klabu hiyo umemalizika au la.
Madeni yanayoikabili klabu
“Nakiri ni kweli tunadaiwa, lakini hakuna taasisi
duniani ambayo haidaiwi, hata Marekani, nchi tajiri inadaiwa, sembuse
Simba, tunajipanga ili kulipa madeni hayo,” alisema Manara.
Alikiri kuwa klabu yao inadaiwa na baadhi ya wachezaji wake iliyovunja nao mikataba, Amissi Tambwe na Donald Mosoti.
Ujio wa kocha mpya na usajili
Akizungumzia kazi ya usajili na kocha mpya, Manara
alisema, kocha mpya atatangazwa ndani ya siku nne kuanzia jana baada ya
uongozi kukamilisha mchujo wa makocha walioomba kuinoa timu hiyo.
“Usajili tunaendelea vizuri, na kweli nilikwenda
kwenye mashindano ya Cosafa (Afrika Kusini) ili kuangalia wachezaji,
mchakato utakapokamilika kila kitu kitawekwa wazi, tutasajili kutokana
na mahitaji yetu msimu ujao na upungufu tuliokuwa nao msimu uliopita ,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment