Nyota
wa timu ya Brazil Neymar alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kipenga cha
mwisho cha mechi ya kinyang'anyiro cha Copa America baada ya timu yake
kufungwa na Colombia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991.
Mshambuliaji
huyo wa klabu ya Barcelona alimpiga mpira Pablo Armero kimakusudi kabla
ya mchezaji wa Colombia Carlos Bacca pia kupewa kadi nyekundu baada ya
kulipiza kisasi kwa kumsukuma Neymar.Beki Jeison Murillo alifunga bao la pekee baada ya dakka 36.Brazil ilijaribu sana kuimarisha mchezo wake lakini ilishindwa kutengeza nafasi za kufunga goli.
Brazil,Colombia na Venezuela wako sawa katika kilele cha jedwali wakiwa na pointi tatu kila mmoja.
0 comments:
Post a Comment