Maafisa wa Palestina wanasema kuwa watu kumi na saba
wa familia moja wameuawa baada ya makombora ya Israel kuharibu nyumba
moja ya ghorofa tatu ya mkuu wa polisi wa Hamas.
Tayseer Al-Batsh anadaiwa kujeruhiwa katika shambulizi hilo.
Mashambulizi hayo yanajiri baada ya
wapiganaji wa Hamas kurusha makombora ya masafa marefu katika miji ya
Israel ikiwemo Tel Aviv.
Maafisa wa Israel wanasema kuwa makombora mawili
ya Roketi yalirushwa kutoka lebanon lakini yakaanguka katika eneo
lililo wazi kazkazini mwa Israeli.
Na katika hatua ya kulipiza kisasi ,Israel
ilirusha makombora nchini Lebanon na kuzidisha hofu kwamba huenda mzozo
huo ukapanuka.
Takriban raia 150 wa Palestina wameuawa katika mashambulizi hayo huku ikiwa hakuna vifo vyovyote vilivyoripotiwa nchini Israel.
0 comments:
Post a Comment