Watu
watatu wamefariki na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa wakati gereza moja
liliteketea moto magharibi mwa Rwanda, karibu na mpaka wa DRC.(Martha Magessa)
Tukio hili linatokea mwezi mmoja baada ya gereza jengine, Muhanga, kuteketea moto katika jimbo lililopo kusini mwa Rwanda.
Ajali
hiyo ya moto imeripotiwa kutokea majira ya jioni (Jumatatu) katika
gereza la Nyakiriba, katika wilaya ya Rubavu mpakani na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
'Uokozi haukutosha'
Rubavu, Rwanda karibu na DRC
Akiongea
na BBC kwa njia ya simu mkuu wa wilaya hiyo, Sheikh Hassan Bahame,
amesema kuwa juhudi za uokozi zimefanyika haraka ila mahabusu 3
walifariki na wengine 44 kupatwa na majeraha ya moto.
Majeruhi walifikishwa mara moja katika hospitali kuu ya wilaya.
Amesema
kuwa kutokana mazingira ya milima ambapo gereza hilo limejengwa, imekuwa
vigumu kwa wazima moto kufanya kazi yao kwa wepesi na haraka.
Shekh
Bhame ameelezea hasara iliyojitokeza.'' Hasara kubwa abayo imetokea ni
kifo cha hawa wafungwa. Na majeraha waliyopata wafungwa wengine. Kuna
vitu vingi vimeharibika na hatujajua idadi yake bado.''
Sheikh
Bahame ametahadharisha kuelekeza lawama la shambulio la kigaidi akisema
kuwa japo inatia shaka, ni muhimu uchunguzi zaidi kufanywa.
''Hata
sisi tunajiuliza, mbona mambo haya yametokea, na juzi tu yametokea
Muhanga?Inatakiwa uchunguzi wa ndani zaidi ufanywe. Lakini uhakika bado
hatujapata.'' Amesema Sheikh Bahame.
Uchunguzi umeanzisha kujua chanzo cha moto, pamoja na ule moto katika gereza la Muhanga mwezi mmoja uliopita.
CHANZO;BBC
0 comments:
Post a Comment