Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akizungumza waandishi wa gazeti la
Mwananchi katika mahojiano maalumu ofisini kwake Makao Makuu ya chama
hicho, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Picha na Edwin Mjwahuzi
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitasubiri wanachama
watakaoachwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uteuzi wa wagombea
katika uchaguzi mkuu ujao.
Kutokana
na tamaa ya kuingiza watu wengi kwenye Bunge, vyama vya upinzani
vimekuwa na tabia ya kuwapokea wanachama wa CCM wanaoshindwa kwenye kura
za maoni na baadaye kuwapa nafasi ya kugombea ubunge, lakini Dk Slaa
anasema safari hii hawatakuwa tayari kufanya hivyo.(Martha Magessa)
"Tulishasema
kwamba kwa ngazi zozote hata ngazi za udiwani au ubunge hatusubiri
mabaki, makapi yatakayotokea CCM ndiyo yaje kwetu," alisema Dk Slaa
katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika makao makuu ya chama
hicho jijini Dar es Salaam.
"Safari
hii hatusubiri. Tulishasema kuwa wagombea wetu tunawaandaa mapema ili
tusitegemee mtu anayekuja dakika za mwisho kuwa ndiyo atuokoe."
Kauli ya
Dk Slaa inaweka msisitizo katika ile iliyowahi kutolewa na mwenyekiti wa
chama hicho, Freeman Mbowe kwamba hawatapokea wanasiasa watakaoihama
CCM ili kupata nafasi za uongozi kwa tiketi ya Chadema.
Katika
mahojiano hayo, Dk Slaa alisema: "Huwezi kuzuia kupokea mwanachama
kokote alikotokea, lakini unapofika wakati wa kuweka watu katika nafasi,
lazima ufikirie."
Mwaka
2010, Chadema ilipokea wagombea wawili walioshindwa kwenye kura za maoni
za CCM, John Shibuda aliyeshindwa katika kura za maoni za Maswa
Magharibi na Freddy Mpendazoe ambaye alienguliwa kwenye kura za maoni za
CCM Jimbo la Segerea.
Shibuda
alifanikiwa kurudi bungeni baada ya kushinda uchaguzi wakati Mpendazoe
alishindwa katika hali ya kutatanisha na juhudi zake za kutengua matokeo
hayo mahakamani ziligonga mwamba.
"Tatizo
hilo lilitokana na ugeni wetu," alisema Dk Slaa akizungumzia kitendo cha
Chadema kupokea wagombea walioshindwa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2010.
"Lakini
kwa wakati huu, Chadema ina wanachama wengi wenye sifa za kugombea hivyo
hatuhitaji kusubiri mtu," aliongea katibu huyo mkuu ambaye aliwahi
kutangaza kuwa nafasi za wagombea ubunge wa Chadema katika majimbo yote
nchini zitatangazwa kwenye magazeti na watakaojitokeza, watafanyiwa
usaili.
Kuhusu
uchaguzi mkuu wa chama hicho, Dk Slaa alisema utafanyika Desemba mwaka
huu baada ya kuridhiwa na kikao cha Kamati Kuu kitakachofanyika Julai
18.
Alisema
wanahakikisha uongozi unapatikana kuanzia ngazi za chini na watachukua
hatua kwa maeneo ambayo watabaini viongozi wamepeana nyadhifa bila
chaguzi madhubuti kufanyika
CHANZO:MWANANACHI
0 comments:
Post a Comment