.

.

Wednesday, 9 July 2014

Wanasoka wana msemo kwamba mpira ni mchezo wa makosa, ndivyo ilivyo na ndo itabaki kuwa hivyo mara timu iapofungwa. Lakini kuna kitu ambacho tunahitaji kukijua ni kutambua kanuni za kusoma mechi, 1.Muktadha wa mechi yenyewe, 2.Historia ya timu hizo, 3. Aina ya wachezaji, 4. Falsafa ya makocha, pengine tunaweza kusema mpira ni mchezo wa makosa vinginevyo vitakuwa ni visingizio vya mfungwaji. Pasi na makosa ya kimchezo Brazir imebaki ni timu ya kihistoria na kama ushindi huwa unapatikana basi ni wa kibahati bahati. Rudia kutizama mechi zao zote tangu wanaanza fainali hizi hakuna mechi ambayo utasema kwamba jamaa hawa wana madhara makubwa langoni mwa timu pinzani, labda tu umuondoe Neyma ambaye alikuwa ndo roho yao bahati mbaya ndo majeraha yakamwandama hata kama angelikuwemo na Silva sana wangepunguza idadi ya magoli. Hivyo wachambuzi wa tuache unazi katika kuiendea mechi wakati wa uchambuzi. MPIRA SI MCHEZO WA MAKOSA.

Silaji Kiwanga's photo.MPIRA SI MCHEZO WA MAKOSA (KIFO CHA AIBU)

0 comments:

Post a Comment