.

.

Saturday, 19 July 2014


Kundi la Alshabaab limeendeleza wimbi la mashambulizi katika mji wa lam nchini Kenya na  limekiri kutekeleza shambulizi katika basi moja la abiria katika pwani ya Kenya hapo jana usiku.
Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu saba walipigwa risasi na kufariki huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Shambulizi hilo lilitokea katika mji wa Witu katika Kaunty ya Lamu.
Watu kadhaa wameuawa katika Pwani ya Kenya katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita.
Kundi la Alshabaab limekiri kutekeleza mauaji hayo.
Linasema kuwa linalipiza kisasi kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini Somali.
Ghasia hizo zimeathiri pakubwa sekta ya utalii nchini Kenya.

0 comments:

Post a Comment