Baada ya kufikisha wachezaji wanne clabuni Chelsea Meneja wa timu hiyo Jose Mourinho amesema hana mpango wa kusajili wachezaji wengine.
Boss huyo amesema amemaliza kununua wachezaji msimu huu
baada ya kukamilisha usajili wa beki wa kushoto Filipe Luis kutoka
Atlètico Madrid.
Luis ni mchezaji wa nne mpya kusajiliwa na Mourinhomsimu huu baada ya Cesc Fabregas, Mario Pasalic na Diego Costa.
"Tumefunga biashara leo," amesema Mourinho. "Dirisha la usajili linafungwa Agosti 31, lakini sisi tumefunga Julai 19.
"Klabu yangu imefanya kazi nzuri, sio kwa wachezaji tulionunua tu, lakini pia kwa sababu tumemaliza biashara mapema kabisa."
Chelsea wamekuwa wakihusishwa na wachezaji kadhaa wa bei ghali msimu
huu, akiwemo Sami Khedira wa Real Madrid na Radamel Falcao wa Monaco.
Saturday, 19 July 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment