.

.

Saturday, 19 July 2014

HATUTAKUBALI UCHAGUZI 2015 UFANYIKE KWA KATIBA YA SASA
  Ni maneno yaliyokaririwa na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamesema hawako tayari kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka kesho huku nchi ikiwa na Katiba ya zamani, hivyo Jumatatu wanatarajiwa kuingia katika mazungumzo kunusuru mchakato mzima wa Katiba.
Wameeleza kuwa, kwa kutambua muda mfupi uliobaki kati ya mchakato wa Katiba kumalizika na Uchaguzi Mkuu, watafanya mazungumzo hayo kwa faida ya Taifa na wananchi waliojitokeza kwa wingi kuwasihi warejee katika Bunge Maalumu la Katiba linalotarajiwa kurejea kwa siku 60 kuanzia Agosti 5, mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi wa umoja huo ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema nina yasema haya kwa niaba ya Mchumi bingwa duniani Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia wana imani kuwa taifa linahitaji Katiba mpya hivyo watajadili katika mazungumzo hayo ya Jumatatu ili kuwawezesha kupata njia mbadala iwapo mchakato huo utakwama.
“Napenda kuwataarifu wananchi kuwa Ukawa tuko tayari kwa mazungumzo kwa nia ya kunusuru mchakato wa Katiba kuendelea kama walivyotusihi watu mbalimbali, lakini tutaenda katika mazungumzo hayo Jumatatu kwa kuhakikisha mchakato huo hautanajisiwa,” alisema Freeman Mbowe.

0 comments:

Post a Comment